Taarifa za kusikitisha zinaeleza kuwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya New Habari wachapishaji wa magazeti ya Mtanzania, Dimba, Bingwa na Dimba, Ndg Absalom Kibanda amevamiwa na watu wasiojulikana akiwa ndani ya gari lake wakati akiingia nyumbani kwake Mbezi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Taarifa zinasema Bw Kibanda alivamiwa majira ya saa sita usiku wa kumkia leo, akitokea kwenye majukumu yake ya kila siku. Inadaiwa kuwa alichomolewa kwene gari yake, akapigwa na vitu vyenye ncha kali kichwani, ameharibiwa jicho lake la kushoto vibaya, pamoja na kunyofolewa kucha na baadhi ya vidole na hatimaye kutupwa umbali kidogo ya nyumbani kwake.
Baada ya hapo wasamalia wema walijitokeza na kumkimbiza Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, ambako alipokelewa vizuri na madaktari na kumpatia tiba ya awali na baadaye kumhamishia Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI) ambako mpaka sasa anaendelea na matibab, kama picha ya juu inavyoonesha.
Inaelezwa kuwa, watu waliomfanyia ukatili huo, hawakuweza kuchukua kitu chochote kwenye gari ambapo kulikuwemo Laptop, simu na nyaraka zingine.
Noize of Silence Blog imepokea taarifa hizi kwa masikitiko makubwa sana. Tunaviomba vyombo vya dola vifanye kila juhudi kuwatia nguvuni wote waliohusika ili sheria ichukue mkondo wake na hatimae iwe fundisho kwa tabia hizi ambazo ni kama zimeanza kuwa kama matukio ya kawaida.
*************************
Wakati huo huo, Handeni Kwetu Blog inaripoti kuwa TASWA wametoa tamko kuhusiana na kujeruhiwa kwa Absalom Kibanda
CHAMA Cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA),inaungana na waandishi wa habari wote kulaani kitendo cha watu wasiojulikana kumvamia na kumjeruhi vibaya mwenyekit wa Jukwaa la wahariri, Absalom Kibanda.
Mwenyekiti wa TASWA, Juma Pinto, alisema kuwa watu hao waliohusika wakamatwe ili sheria ichukue mkondo wake.
Tusingependa Kama waandishi kuamini yanayosemwa lakini kutokana na uadilifu mkubwa wa vyombo vyetu vya ulinzi na Usalama kuwapata watu ambao wamehusika na tukio hilo.
Sisi tunaamini tukio hili la mwenzetu kuvamiwa na watu hao halikuwa kwa bahati mbaya ni Jambo ambalo linaonekana Kama limepangwa na Kama ni hivyo lengo na madhumuni yake ni nini kwa waandishi wa Tanzania? Uhuru na Usalama wa waandishi upo wapi?
Kutokana na tukio hili la mpiganaji na Kiongozi wetu kuvamiwa ,ipo haja ya sisi waandishi kuungana pamoja katika kutafuta Usalama wetu.kuna matukio mengi ya waandishi yametokea na tumekuwa tukipiga kelele lakini matokeo yake hakuna hatua ambazo serikali inayafanyia kazi.
Kutokana na majeraha makubwa aliyopata mwenzetu,tunaiomba serikali na hats Mheshimiwa Rais,Dr Jakaya Kikwete kutoa Masada wa mwenzetu kwenda kutibiwa nje,tunaamini serikali ni sikivu na Rais wetu ni mwenyeji kusikia kilio cha watu wake.
Kibanda na wenzake ndani ya Jukwaa la Wahariri wamekuwa mstari wa mbele katika kurudisha hadhi ya tasnia ya habari na kujenga umoja miongoni mwa waandishi wa habari na kuifanya tasnia ya habari kuheshimika tofouti na ilivyokiwa nyuma.
Tunaungana na kampuni ya Habari, wafanayakazi wenzake, familia yake na waandishi wote kwa jumla na kumuomba Mungu ampomye ili tuweze kuunganae nae katika kusaidia kupasha habari Watanzania lakini ili aweze kuwaongoza waandishi wenzake
0 maoni:
Post a Comment