Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

MAELEFU WAJITOKEZA KUMUAGA ALIYEKUWA RAISI WA VENEZUELA HAYATI HUGO CHAVEZ, WENGINE WASHINDA BAR KUSHEREHEKEA KIFO CHAKE.

Mwili wa Chavez ukipitishwa katika barabara za mji mkuu Caracas

Mwili wa Chavez umelazwa katika kituo cha mafunzo ya kijeshi mjini Caracas na marais wa nchi jirani walifika kutoa heshima zao za mwisho akiwemo Rais wa Bolivia Evo Morales na mwenzake wa Argentina Cristina Fernandez de Kirchner.Mama yake na watoto wake walikusanyika mbele ya jeneza kutoa heshma zao .

Kifo chake kilitangazwa na serikali ya Venezuela Jumanne wiki hii

Mwaka uliofuata Chavez alichaguliwa na wananchi kuongoza kwa muhula wwingine wa miaka sita kuiongoza Venezuela .Watu wengi waliangua kilio huku wakichukua picha za kiongozi wao aliyefariki dunia .

Mwaka 2011 Chavez alisema kuwa anapokea matibabu ya Saratani nchini Cuba

Chavez alionekana kama mpigania haki za watu maskini kwa kusisitiza sera zake za kisosholisti na kuzichanganya na demokrasia.

Mwili wa Chavez ulipitishwa katikati ya mji mkuu Caracas na kusindikizwa na maelfu ya watu waliomuunga mkono,Watu wengi waliangua kilio huku wakichukua picha za kiongozi wao aliyefariki dunia .

Chavez alikuwa na maadui wengi pamoja na wale waliomuona kama mwokozi wao kwa sababu ya sera zake za kisosholisti.Watu wengi waliangua kilio huku wakichukua picha za kiongozi wao aliyefariki dunia .

Hugo Chavez hakupendwa na kila mtu Venezuela wakati wa utawala wake.Wapinzani wa Hugo Chavez wakisherehekea katika moja ya kumbi za maburudiko baada ya kupokea habari za kifo chake mjini Florida, Marekani. Picha Kwa Hisani ya Reuters na AFP

……………………………………………………..

Mwili wa mareheu rais Hugo Chavez wa Venezuela, umelazwa katika kituo cha mafunzo ya jeshi katika mji mkuu Caracas Mapema leo mwili wa marehemu Chavez ulipitishwa kwenye umati mkubwa wa wafuasi wake katika mitaa ya mji mkuu Caracas. Watu wengi waliangua kilio huku wakichukua picha za kiongozi wao aliyefariki dunia.Mama yake na watoto wake walikusanyika mbele ya jeneza kutoa heshma zao .

Makamu wa rais Nicolas Maduro anaongoza shughuli hiyo. Mwili wa rais Chavez umepelekwa katika chuo cha kitaifa cha mafunzo ya kijeshi ambapo utazikwa kesho Ijumaa. Bwana Chavez alifariki akiwa umri wa miaka 58 baada ya kuugua Saratani kwa zaidi ya miaka miwili. Maelfu ya watu awali walikwenda barabarani mjini Caracas kutoa heshima zao za mwisho kwa Chavez wakifuatana na gari lililokuwa limebeba jeneza lake kuelekea katika chuo cha mafuzno ya jeshi.

Mazishi ya kitaifa ya Chavez yatafanyika Ijumaa. Mkuu wa ulinzi wa Rais alinukuliwa akisema kuwa alikuwa na bwana Chavez alipofariki. Generali Jose Ornella, alisema kuwa Chavez alifariki kutokana na mshtuko wa moyo na katika siku zake za mwisho kabla ya kifo cha ealisema angependa kuendelea kuishi. Jeneza lake lililokuwa limefunikwa bendera ya nchi hiyo uliwekwa katika ukumbi ambao ni kumbukumbu ya waliopigania uhuru wa watu wa Amerika ya Kusini

Maelfu ya watu walipanga foleni kutoa heshima zao za mwisho kwa marehemu Chavez, wakiwemo maafisa wa serikali na viongozi wa Amerika ya Kusini,kama Rais wa Bolivia Evo Morales na Rais wa Argentina Cristina Fernandez de Kirchner.

Chanzo: BBC SWAHILI, ALHAMIS, MACHI 07, 2013

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO