Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Taswira: Mapokezi ya Rais Xi Jinping wa China Jijini Dar es Salaam Jana

Rais wa China, Mhe. Xi Jinping, Rais Kikwete na wake zao wakiwapungia mkono wananchi mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam kwa Ziara ya Kitaifa ya siku mbili hapa nchini.

Rais wa China, Mhe. Xi Jinping na mke wake wakiteremka kwenye ndege mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam kwa Ziara ya Kitaifa ya siku mbili hapa nchini.

Mhe. Rais Xi Jinping na Mhe. Rais Kikwete wakiwa katika Jukwaa Maalum wakati nyimbo za mataifa yao zilipokuwa zikipigwa sambamba na mizinga 21 kwa heshima ya Mhe. Rais Xi Jinping.

Mhe. Rais Xi Jinping akikagua Gwaride Maalum lililoandaliwa kwa heshima yake.

Mhe. Rais  Xi Jinping na mwenyeji wake Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiwasalimia baadhi ya kina mama wa Dar es Salaam waliofika Uwanjani hapo kwa ajili ya mapokezi.

Mhe. Rais Xi Jinping na mwenyeji wake Mhe. Rais Kikwete kwa pamoja na wake zao wakifurahia burudan iliyokuwa ikitolewa  na moja ya viku ndi vya burudani vilivyokuwa uwanjani hapo mara baada ya Rais Xi Jinping kuwasili nchini.

Mhe. Rais Xi Jinping na Mhe. Rais Kikwete wakiondoka uwanjani hapo mara baada ya mapokezi.Picha Zote na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa


PICHA: HAKINGOWI.COM NA MUHIDIN MICHUZI

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO