Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

MAZISHI YA ALIYEKUWA MJUMBE WA BARAZA KUU LA UVCCM KUFANYIKA LEO JUMA TANO NYUMBANI KWAO DARAJA MBILI JIJINI ARUSHA

DSCF8052

Waombolezaji mbalimbali wakiwemo viongozi wa vyama wakilia kwa uchungu nyumbani kwao marehemu  jana ,,aliyeinamisha kichwa chini mwenye hanjifu ni Mwenyekiti UVCCM mkoa Arusha Robson Meitinyiku

DSCF8059

Mama mzazi wa marehemu Bi.Suzan Mollel akiwa katika majonzi makubwa

DSCF8054

Baadhi ya Waombolezaji nyumbani kwao marehemu

TUKIO la kufariki kwa aliyekuwa mjumbe wa baraza kuu la Uvccm mkoani Arusha,Benson Mollel(26) limevuta hisia kwa wakazi wengi wa jijini Arusha mara baada ya vifaa mbalimbali kama silaha aina ya bastola,kadi za benki,simu na fedha ambazo kiasi chake hakijajulikana kukutwa katika chumba cha marehemu ndani ya hoteli ya Lush Garden Business iliyopo jijini hapa

Mbali na kujishughulisha na siasa marehemu pia alikuwa akifanya kazi katika kampuni ya madini ya Manga Gems iliyopo jijini Arusha ambapo ndani ya chumba alichofia alikuwa silaha aina ya bastola,madini ya tanzanite,simu mbili ,kadi za benki na fedha ambazo kiasi chake hakijulikani.

Hatahivyo,utata mzito  umezidi kugubika katika kifo cha marehemu huyo mara baada ya mipira miwili ya kiume(condoms) ambapo mmoja ukiwa umetumika kukutwa katika eneo la tukio.

Marehemu Mollel alikutwa amefariki majuzi ndani ya hoteli ya Lush Garden Business iliyopo mtaa wa Jacaranda jijini Arusha katika mazingira ya kutatanisha huku mwili wake ukiwa uchi  wa myama na mipira miwili ya kiume(condoms) ambapo mmoja ukiwa umetumika kukutwa katika eneo la tukio.

Mashuhuda wamesema kabla ya marehemu kukutwa na mauti alitembelewa na wanawake wawili kwa nyakati tofauti ndani ya chumba chake ambapo mmoja ametambulishwa kwa jina la Nancy na mwingine Mariam.

Kwa upande wake mwenyekiti wa CCM wilaya ya Arusha,Dk Wilfred Ole Soilel alisema kuwa chama chao kimepokea msiba huo kwa masikitiko makubwa kwa kuwa marehemu alikuwa anatumia busara za kuwaunganisha vijana ndani ya chama hicho kwa ukarimu.

DSCF8049

Hoteli aliyofia marehemu

DSCF8044

Gari la Marehemu alilotumia kufika hotelini hapo ambapo kabla ya umauti kumkuta aliegesha gari hilo nyuma ya hotel

PICHA NA JAMII BLOG, ARUSHA

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO