Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Lowassa aingia Karatu, achangisha mil. 200/-

WAKATI Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa alichangisha zaidi ya sh milioni 200 fedha taslimu na ahadi katika harambee ya ujenzi wa chuo cha afya wilayani hapa, kiongozi huyo amesifiwa kwa uthubutu wa kuagiza na kutenda.

Sifa hizo zilitolewa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Karatu na Diwani wa Kata ya Ganako, Lazaro Maasai (CHADEMA) wakati wa harambee ya chuo hicho kinachomilikiwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Karatu kwa ushirikiano na serikali.

“Wewe ni Waziri Mkuu pekee uliyekuwa unathubutu na kutekeleza kwa vitendo,” alisema Maasai huku akikumbushia jinsi alivyosimamia ujenzi wa shule za sekondari za kata nchini.

Alisema ile ndoto yake ya kuwaendeleza Watanzania kielimu, Karatu waliifanyia kazi na ndiyo maana wanajenga chuo hicho cha afya ili wale watoto wanaomaliza kidato cha nne waweze kuendelea na masomo.

Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini Dk. Martine Shao, akizungumza katika ibada hiyo alimshukuru Mungu kwa kujibu maombi yao.

Alisema siku zote kanisa huwa halibahatishi, na kwamba anaamini Mungu amempa Lowassa vipaji mbalimbali.

“Mungu amekubariki na ndiyo maana ukitoa kauli nchi nzima inafuata na kote ulikofanya kazi tumeona kazi yako, Watanzania wanamshukuru Mungu.

“Siku zote mtu mwenye vipaji ana ndoto nyingi, umesimamia ndoto zako vizuri, hatujui huko mbele tuendako, tunamuomba Mungu akulinde na kukubariki katika wajibu wako,” alisema.

Lowassa akizungumza kabla ya kuanza kuchangisha, aliwaeleza waumini hao kwamba zipo sababu kadhaa ambazo zimekuwa zikimsukuma kutumika katika harambee.

Tanzania Daima

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO