Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Muasi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Jenerali Bosco Ntaganda, amejisalimisha katika ubalozi wa Marekani mjini Kigali, Rwanda.

Hatimae Marekani imethibitisha kuwa Muasi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Jenerali Bosco Ntaganda, amejisalimisha katika ubalozi wake mjini Kigali, Rwanda.

Taarifa hiyo ya Marekani inasema kuwa Ntaganda ameomba ahamishwe hadi katika Mahakama ya Uhalifu wa Kimataifa ICC huko the Hague.

Ntaganda aliyeanzisha maasi nchini Congo ameshitakiwa katika mahakama hiyo ya ICC na anakabiliwa na mashitaka ya kuwajumuisha watoto katika jeshi, mauaji na ubakaji.

Jenerali Ntaganda mwenyewe anakanusha madai hayo yote.

Marekani imesema kwa wakati huu inashauriana na serikali kadhaa ili kufanikisha ombo hilo la Jenerali Ntaganda ahamishwe hadi mahakama ya ICC.

Awali Serikali ya Rwanda ilikuwa imetangaza kuwa Jenerali huyo muasi anayetuhumiwa kuhusika na uhalifu wa kivita katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo amejisalimisha katika ubalozi wa Marekani mjini Kigali, Rwanda.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda Louise Mushikiwabo amesema taarifa walizonazo ni kuwa Kiongozi huyo muasi yuko chini ya ulinzi wa Marekani katika ubalozi wake.

"Tumefahamishwa hii leo (Jumatatu) kuwa Bosco Ntaganda ameingia Rwanda na kujisalimisha katika Ubalozi wa marekani hapa Kigali", amesema Louise Mushikiwabo

Jenerali Ntaganda amekanusha mashitaka yanayomkabili katika mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Jinai ICC kwamba anahusika na uhalifu wa kivita na ule dhidi ya binadamu

BBC Swahili

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO