Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimesaini mkataba wa ushirikiano na Chama cha Conservative cha watu wa Denmark. Mkataba huo una lengo la kuwajengea uwezo Vijana na Wanawake zaidi ya 30,000 kwa njia ya mafunzo mbalimbali kupitia mabaraza yao ya Vijana na Wanawake.
Mkataba huo utagharimu takribani kiasi cha Tsh Milioni 400. Akisaini Mkataba huo mbele ya Waandishi wa Habari KatibuMkuu wa CHADEMA Dr. Wilbrod Slaa amesema wamefanya shughuli hiyo mbele ya waandishi wa habari na kuweka hadharani mkataba huo ili kuonyesha uongozi wamfano kwani CHADEMA imekuwa ikiitaka mikataba yote inayosainiwa kwa niaba yaWananchi kuwekwa hadhari ili wananchi waweze kuitambua na kuielewa.
Dr. Slaa ameongeza kuwa wanafanya mambo yao kwa uwazi ilikuepuka propaganda zinazofanywa na serikali kupitia usalama wa taifa pamoja na Chama Cha Mapinduzi juu ushirikiano ambao CHADEMA imekuwa ikiupata kutoka kwavyama rafiki duniani. CHADEMA ni mwanachama wa umoja wa vyama vya kidemokrasia duniani unaojulikana kama IDU.
Walioshuhudia utiaji huo wa saini ni Makatibu wakuuwa Baraza la Vijana Deogratius Munishi na wa Baraza la Wanawake Naomi Kaihula.Wengine ni Wakurugenzi na Maafisa mbalimbali wa CHADEMA Makao Makuu
0 maoni:
Post a Comment