Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Taswira: Mkutano wa Chadema Jijini Arusha viwanja vya Ngarenaro Mei 2, 2013

DSC06339Mbunge wa Arusha Mjini Mh godbless Lema akihutubia maelfu ya wananchi wa Arusha waliojitokeza katika Mkutano wa Chadema uliofanyika katika uwanja wa Shule ya Msingi Ngarenaro Alhamisi ya tarehe 2 Mei, 2013. Mbali na Lema, mkutano huo ulihubiriwa pia na James Ole Millya na viongozi wengine wa chama. Katika mkutano huo wanachama kadhaa wa Chadema walitambulishwa kama miongoni mwa watu waliojitokeza kuwania nafasi ya kuteuliwa na chama hicho kugombea nafasi nne za udiwani zilizowazi Jijini hapa.

DSC06329James Ole Millya akihutubia mkutanoni hapo ikiwa ni siku moja tu tangu habari zisambazwe mitandaoni kuwa amekimbilia Oman alikoajiriwa, jambo ambalo mwenyewe alikanusha na kuieleza Blog hii kuwa alikwenda kwa shughuli zake za biashara.

DSC06327Mzee huyu alikuwa kivutio sana kwenye mkutano huo

DSC06311Mh Lema akilakiwa na viongozi wengine wa chama wakati akiwasilia viwanjani hapo

DSC06315James Millya akisalimiana na kamanda Magoma J Magoma aliyejitambulisha kuwa anania ya kuwania udiwani Kata ya Kimandolu.

DSC06333

DSC06313Benchi kuu

DSC06320Kalist Bush akisalimiana na James Millya

DSC06317Baadhi ya vijana waliotangaza nia kuwania nafasi za udiwani

DSC06342Picha nzuri ya wanaChadema wakifuatilia mkutano wa chadema huku wakiburudika na juice za Bakhresa. Kutoka kulia, Doris Cornelly, kiongozi wa Bavicha Wilayani Hai, anafuata Glory Kaaya, Katibu wa Bavicha Wilaya ya Arusha na Exaud Mamuya, Mwenyekiti mstaafu Bavicha Wilaya ya Arusha Mjini.

DSC06334Picha zote na Seria Jr

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO