Aliekuwa mgombea wa CHADEMA, Mwalimu Norbet Yamsebo akiwa na furaha mara baada ya kuibuka mshindi
Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga kutengua matokeo ya ubunge wa jimbo la Sumbawanga mjini yaliyompa ushindi mgombea wake Aeshi Hilal.
Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya, Betwell Mmila, alitengua matokeo ya mbunge huyo baada ya kubaini kuwapo kwa dosari katika ya vipengele kadhaa wakati wa mchakato wa uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 31, 2010.
Kati ya hoja 21 zilizowekewa pingamizi na aliyekuwa mgombea ubunge kupitia CHADEMA, Nobert Yamsebo (pichani juu), ni vipengele viwili pekee ambavyo mahakama hiyo imeridhia kuwa na dosari katika uchaguzi huo.
Mamia ya wafuasi wa CHADEMA waliofurika ofisi ya chama mara baada ya hukumu iliyotengua matokeo ya Ubunge wa Hilary Aeshi wa CCM (Picha na Mdau Meddy Arfi, Sumbawanga)
Kutoka Biharamulo…
Habari tulizozipata na kuthibitishwa na Mh.Conchesta Rwamlaza MB CHADEMA,ni kuwa Dkt.Anthony Mbasa ameshinda kesi dhidi ya maombi ya kutenguliwa ubunge wake. Katika hali isiyokuwa ya kawaida Jaji alichelewa sana kuingia mahakamani,na hukumuimesomwa mfululizo hadi usiku. (Chanzo: Mjengwa Blog)
0 maoni:
Post a Comment