Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

ABDULHAMAN KINANA KATIBU MKUU WA CCM

Mkutano mkuu wa Chama Cha Mapinduzi NEC mjini Dodoma, umempitisha Abdulhaman Kinana kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho tawala.
Mwenyekiti wa CCM, Mh Jakaya Kikwete alishamteua Katibu Mkuu wa zamani, Philip Mangula, kuwa Makamu Mwenyekiti, akirithi mikoba ya Pius Msekwa.

Naye Mwigulu Nchemba amechaguliwa kuwa naibu katibu mkuu wa chama hicho upande wa bara na Vuai Ali Vuai upande wa Tanzania visiwani.
Wengine waliofanikiwa kupita kwenye secretarieti ya chama hicho ni pamoja na Asha Rose Migiro ambaye amechaguliwa kushughulikia masuala ya kimataifa na Zakhia Meghji amechaguliwa kushika nafasi ya uweka hazina.
Nape Nnauye ameendelea kushikilia nafasi yake katibu na uenezi wa chama hicho.

Abdurahman Kinana-Katibu Mkuu wa CCM

Mwigulu Nchemba-Naibu Katibu Mkuu CCM (Bara)

Vuai Ali Vuai-Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar)

Nape Nnauye-Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi

Asha-Rose Migiro-Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa

Zakia Hamdan Megji- Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha

Muhammed Seif Khatib-Katibu wa NEC, Oganaizesheni.
Picha zote kwa hisani ya Bashir Nkoromo













Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO