Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

SHEREHE ZA MEI MOSI JIJINI DAR ES SALAAM LEO; KITAIFA JIJINI MBEYA AMBAKO JK NI MGENI RASMI

Baadhi ya wafanyakazi kutoka Wizara mbalimbali za Serikali na Taasisi Binafsi wakiwa katika foleni wakijiandaa kuanza maandamano kuelekea kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja kwa ajili ya kushiriki maadhimisho ya Sherehe za Mei Mosi, ambapo katika Sherehe hizo mgeni rasmi alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Saidick, huku sherehe hizo kitaifa zikifanyika Kitaifa Mkoani Mbeya, na Mgeni Rasmi huko ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.

Mgeni rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadick, akiwa meza kuu na baadhi ya viongozi wengine wakati wakisimama kupokea maandamano hayo.

Wafanyakazi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii NSSF, wakipita mbele ya jukwaa kuu na maandamano na mbwembwe za kucheza Kiduku, wakati wa sherehe hizo.

Wafanyakazi wa TALGWU, wakipita mbele ya jukwaa kuu na Bango lenye ujumbe.

Twiga Cement wao walikuwa wakipromoti bidhaa yao tu bila hata bango lenye ujumbe kuhusiana na sherehe hizo.

Maandamano yakiendelea kupita mbele ya jukwaa kuu.

Maandamano yakipita mbele ya jukwaa kuu........

Watu wa Mahakama wakipita na bango lao mbele ya jukwaa kuu..

PICHA NA MITANDAO

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO