Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

AY balozi mpya Airtel

KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel, imemtangaza msanii wa muziki wa kizazi kipya, Ambwene Yesaya ‘AY’ kuwa balozi wake mpya kwa mwaka 2012-2013.

Airtel imekuwa na utaratibu wa kushirikiana na wasanii nchini ili kufanya shughuli mbalimbali za kijamii.

AY kati ya wasanii mahiri ndani na nje ya nchi, aliyejipatia heshima na kuvuta hisia za wapenda burudani wengi, alitangazwa jana katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando, wameingia makubaliano na AY kuwa balozi wao wa mwaka huu.

Alisema jana kuwa, lengo ni kuendelea kuwa karibu zaidi na wasanii wa hapa nchini, pia kufanya nao shughuli za kijamii kwa manufaa ya taifa.

“Sasa AY atakuwa ni msanii wa pili kuingia mkataba kama huu. Mwaka uliopita alikuwa Ali Kiba. Tulimtangaza Ali Kiba kuwa balozi wa Airtel mwaka jana na ameshirikiana na Airtel kikamilifu katika shughuli mbalimbali za kuitangaza kupitia matangazo ya redio, runinga, mabango na mabandiko.

“Lakini pia alifanikiwa kuiwakilisha nchi yetu kwenye wimbo wa ‘Hands Across the World’ alioimba na wasanii wengine wa kimataifa akiwemo R. Kelly katika kundi la One8 kwa udhamini wa Airtel na kufaulu sana kubainisha umahiri wa wasanii wa Tanzania kwenye mataifa mengine makubwa kupitia kazi yake nzuri aliyofanya ndani ya wimbo huo,” alisema Mmbando.

AY ni msanii aliyewahi kufanya matamasha ya kimataifa katika nchi mbalimbali kama Marekani, Uingereza, Hispania, Dubai, Burundi, Rwanda, Ethiopia, Malaysia, India, Russia, Afrika Kusini, Kenya na Uganda.

Aidha, ni msanii mwenye rekodi nzuri ya kufanya kazi na wasanii mbalimbali wa kitaifa na kimataifa.

Kwa upande wa wasanii wa kimataifa waliowahi kufanya kazi na AY, ni Chameleon na Ngoni wa Uganda, Amani, Nameless, Jua Cali (Kenya), P. Square, J. Martins (Nigeria), Ms. Trinity, Sean Kingston anayewika Jamaica na Lil Romeo wa Marekani.

Pia, AY ni msanii wa kwanza wa kiume Tanzania, kutunukiwa tuzo ya KORA mwaka 2005 na kupata pia tuzo ya MTV MAMAs ya 2009 na France Awards mwaka 2010.

Kwa sasa amechaguliwa katika kuwania tuzo za Channel O katika vipengele vitatu vya video bora ya Afrika, video bora ya mwaka na mwanamuziki bora wa kiume wa mwaka.

Akizungumzia uteuzi wake, AY kama balozi wa Airtel, alisema kwa kushirikiana na kampuni hiyo atakuwa akifanya shughuli za kijamii, hususani katika kuchangia ukuaji wa elimu nchini.

“Kwa kushirikiana na Airtel, tutaandaa maonyesho mbalimbali ya burudani kwa ajili ya wateja wetu na hii itatangazwa hivi karibuni.

“Na kwa kuanza kama balozi wa Airtel, napenda kuwaomba na kuwahimiza Watazania wenzangu kuweza kuchangia mradi ambao tumeshauanzisha wiki tatu zilizopita tukishirikiana na BAMVITA katika kuchangia vitabu kwa ajili ya watoto wenye mahitaji maalumu,” alisema

Source: Tanzania Daima

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO