TANZANIA inatarajiwa kuwa mwenyeji wa mkutano wa Jukwaa la mapinduzi ya kijani Afrika( AGRF) utakaofanyika kuanzia septemba 26 hadi septemba 28 mjini Arusha utakaokutanisha viongozi mbali mbali wa kimataifa ambao watajadili namna ya kuchukua hatua katika kuboresha usalama wa chakula duniani .
Aidha katika mkutano huo viongozi hao wataweza kujadili sera ya mapinduzi ya kilimo na uchumi wa Afrika ,njia za kukuza masoko pamoja na namna ya kubadilisha mfumo wa kilimo.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa Rais wa umoja wa mapinduzi ya kijani Afrika (AGRA) bi Jane Karuku alisema kuwa mkutano huo ni hatua inayofuata katika kuendeleza bara la Afrika kupata ufumbuzi katika masuala ya usalama wa chakula.
Karuku alisema kuwa Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano huo katika kukuza sekta ya ukuaji wa kilimo inawakilisha uchunguzi uliofanywa katika wilaya ya kilombero mkoa wa morogoro juu ya njia bora za kilimo.
Alieleza kuwa uchunguzi huo uliwezesha uzalishaji wa mahindi kwa wakulima wadogo wa wilaya hiyo kuongezeka kutoka tani 1.5 hadi 4.5 kwa hekta ,ambapo kwa upande wa mavuno ya mpunga yaliongezeka kutoka tani 2.5 hadi tani 6 hali iliyopelekea Tanzania kupata fursa hii ya kuwa mwenyeji wa mkutano huo.
Aidha alisema kuwa jukwaa hilo litatoa nafasi ya kujadili namna bora ya kuendeleza mipango ya uwekezaji wenye tija kwa ajili ya kuongeza maendeleo ya kilimo barani Afrika pamoja na kujadili namna bora ya kuunganisha nguvu ya jamii na sekta binafsi katika kuboresha usalama wa chakula duniani
Aliongeza kuwa jukwaa hilo pia litaweza kujadili na kutafuta njia bora za kuboresha kilimo barani Afrika na kuwawezesha wakulima wadogo wadogo kushirikiana na vyama vya ushirika na wadau wengine ambapo mjadala huo utatoa njia bora za matumizi ya rasilimali na kukabiliana na changamoto zinazowakabili mamilioni ya wakulima barani Afrika.
“Wakulima wadogo wadogo ni kitovu kwa yale yote tuyafanyayo hivyo mtazamo wetu ni kuwapatia wakulima wa afrika dhana za kilimo wanazohitaji ili waweze kukua zaidi na kuongeza kipato chao na watatuongoza katika kupata mafanikio mazuri”Alisema bi Jane.
Hata hivyo aliwataja viongozi wa kimatiafa watakaoudhuria mkuano huo kuwa ni pamoja Melinda Gates mwanzilishi wa co-melinda Gates rais wa IFAD Dk Kanayo Nwanze ,waziri wa kilimo wa Nigeria Dk Akinwumi Adesina ,mshindi wa tuzo ya chakula Prof .Gebisa Ejeta pamoja na rais wa shirika la kimataifa la Yara International Jorgen Ole Haslestad.
Source: Bashir Nkoromo; Imeandikwa na Rose Jackson, Arusha
0 maoni:
Post a Comment