Mwenyekiti wa chama cha wananchi CUF na mchumi mahiri duniani, Prof Ibrahimu Lipumba akimtambulisha Ndg John Bayo ambae aliwahi kuwa Diwani wa Kata ya Elerai Jijini Arusha kabla ya kuvuliwa uananchama wa chama hicho na Kamati Kuu kufuatia kuingia muafaka na CCM akiwa na madiwani wengine 4, muafaka ambao haukuafikiwa na chama kuhusiana na sakata la uchaguzi wa meya wa Manispaa ya Arusha.
Hata hivyo, kuhamia kwake CUF sio rekodi mpya katika maisha yake ya kisiasa kwasababu ameelezwa kuwa miongoni mwa waasisi wa chama hicho mkoani hapa na alishiriki kutafuta wadhamini wakati wa usajili wa chama hicho. kwa hiyo ni kama anarudi alikowahi kuwa zamani.
CUF leo walikuwa na mkutano wenye sura ya kitaifa katika viwanja vya Levolosi Jijini Arusha kwa maana kwamba viongozi karibu wote wa kitaifa walihudhuria mkutano huo sambamba na msafara wa wanachama zaidi ya 300 kutoka Dar es Salaam. Miongoni mwa viongozi waliohudhuria mkutano huo ni pamoja na Prof Lipumba, Katibu Mkuu Maalim Seif S hamad ambae pia ni Makamu wa Rais Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar.
Wengine ni Naibu Katibu Mkuu bara, Julius Mtatiro, Makamu Mwenyekiti, Machano Ally na viongozi wengine wengi wakiwemo mawaziri wa chama hicho katika SUK Zanzibar.
Swala la madiwani wa Arusha, zinazodaiwa kuwa vurugu za kisiasa, udini katika siasa, utawala mbovu wa CCM na Chadema kwa ujumla ni miongoni mwa masuala yaliyozungumzwa katika mkutano huo.
Kwa upande mwingine chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) wao walikuwa na Mkutano wao katika Kata ya Sombetini ambapo alikuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Mh Lema alihutubia na kuuza kadi za chama kwa mamia ya watu waliojitokeza katika mkutano huo. Lema amekata rufaa kuvuliwa ubunge na rufaa hiyo inatarajiwa kusikilizwa Jumanne ijayo, Oktoba 2, 2012.
Meza ya viongozi wakuu wa chama cha wananchi CUF
Sehemu ya Jukwaa Kuu la viongozi waalikwa
Hoyce Temu akirukaruka ishara ya mchakamchaka kusalimia wapenzi wa CUF.
Naibu Katibu Mkuu Bara, Julius Mtatiro akizungumza katika kkutano huo leo
Katibu Mkuu wa CUF na Makamu wa Rais Zanzibar, Maalim Seif akizungumza
Mwenyekiti wa chama hicho Prof Lipumba akifafanua jambo katika mkutano wa leo Arusha
Sehemu ya wananchi waliokuwa wakisikiliza hotuba za viongozi. Kuna taarifa za kuaminika zinaeleza kuwa miongoni mwa waliohudhuria mkutano huu kuna watu zaidi ya 300 waliotoka Dar es Salaam, morogoro na Tanga wakitumia usafiri wa mabasi madogo 10 yenye uwezo wa kubeba watu 30 kila moja. Nao walikuja kushuhudia uzinduzi wa mchakamchaka wa CUF kuelekea 2015 kwa upande wa Arusha.
0 maoni:
Post a Comment