Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Mshindi wa BSS 2009, Paschal Cassian kukusanya milioni 30 kusaidia machangudoa wa uwanja wa Fisi

MSHINDI wa shindano la BSS 2009 Paschal Cassian amepania kukusanya shilingi milioni 30 kwa ajili ya kupambana na biashara ya uuzaji wa miili inayofanywa na machangudoa wa uwanja wa Fisi.

Cassian alisema hayo wakati akizindua albamu yake ya nyimbo za injili iitwayo  Yasamehe Bure,  yenye nyimbo nane.

Nyimbo hizo ni  Chuki ya Nini, Nikumbuke na Mimi, Jina la Yesu, Mafuriko, Pesa, Baba na Usilie.

Kama ilivyo kawaida katika uzinduzi wa nyimbo za injili huwa kunakuwa na wakati wa kuchangisha fedha za kununulia albamu husika ambapo katika tukio hilo MC alianza kwa kuelezea uuhimu wa kuchangia albamu hiyo.

Mbali na kufafanua kwa inalenga kuwasaidia akinadada wanaojiuza lakini pia alisisitiza kuwa akinadada hao watapatiwa njia mbadala ya kuondokana na sakata hilo.

Naye Jaji Mkuu wa shindano la Epiq Bongo Star Search (EBSS) Ritha Paulsen aliyekuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo alipopanda jukwaani alianza kwa kumkosoa MC kwa kusisitiza kuwa inatakiwa hata hao wanunuaji kwa maana ya wanaume kuacha kununua mara moja.

Alisema kuwa ili kupambana na biashara hiyo haramau inatakiwa kwanza wanaume kuepuka kwenda kununua madada hao kwa kuwa wanunuzi wasipokuwepo basi hata wauzaji hawatakuwepo.

Pia alichangia albamu hiyo kwa kuinunua kwa milioni 10 ili kufanikisha kampeni hiyo muhimu.

Naye Cassian alichangia kwa kusema kuwa akiwa kama kijana mbali na kumtumikia Mungu kwa kila jambo pia ameona kuwa ni wakati muafaka wa kuwatumikia wanadamu ambao ameanzia kwa wanadada hao wa Uwanja wa Fisi.

Uzinduzi huo ulihudhuriwa na maelfu ya watu waliojitokeza katika eneo hilo huku wengine wakiwa wanaimba nae na kucheza nae pamoja.

Akizungumzia zaidi albamu hiyo alisema kuwa ina lenga kuwarudisha waliopotea kwa Mungu kwa kuwapatia ujumbe wa neno la Mungu kwa njia ya nyimbo.

Jaji Mkuu wa shindano la Epiq Bongo Star Search (EBSS), Ritha Paulsen (katikati) akikata utepe kuzindua albamu ya mshindi wa shindano la BSS 2009 Paschal Cassian (kulia).

Paschal Cassian akikamua vilivyo wakati wa uzinduzi wa albamu yake uliofanyika uwanja wa Fisi jijini Dar.Madam Rita akichangisha fedha za kwa ajili ya huduma ya kuwasaidia machangudoa wa Uwanja wa Fisi.

CHANZO: HABARI MPASUKO BLOG

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO