Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

MILLYA:TANZANITE HAIJAWASAIDIA WAKAZI WA SIMANJIRO.

SAM_2873Aliyekuwa mwenyekiti wa vijana wa umoja wa vijana cha cha mapinduzi (ccm) mkoa wa Arusha, James Ole Millya ambaye sasa ni kada wa chama cha demokrasia na maendeleo chadema (chadema) amesema madini ya Tanzanite, yanayochimbwa simanjiro bado hayajawanufaisha vijana wa eneo hilo kielim na kiajira na kuwapa wananchi mazingira bora ya ufugaji.
"Tanzanite inatakiwa kuwanufaisha kwanza vijana wa Wilaya hiyo ya simanjiro mkoani Manyara kufanya hivyo siyo ubaguzi bali ni kutumia rasilimali tuliojaliwa na mwenyezi mungu kujiendeleza na kuboresha maisha yetu” alisema.
Alisema hayo mwishoni mwa wiki iliyopita, wakati akitangaza azma yake ya kuwania ubunge wa jimbo la Simanjiro katika uchaguzi mkuu utakaofanyika nchini mwaka 2015 kwa tiketi ya chadema.
Alisema kwa upande wa Mererani lilippaswa kuwa ni moja ya maeneo tajiri kutokana na Tanzanite lakini hali ni tofauti kwani wakazi wake kwenye umaskini wa kutupwa kiasi kwamba wapo wasiomudu milo miwili kqa siku huku wakazi wa Jaipur nchini India yanayosafirishwa madini hayo kwa wingi wakiishi maisha bora.
"Tanzania yenye utajiri wa madini kama Tanzanite, mlima wa pili kwa urefu duniani, mbuga za wanyama,gesi na rasilimali kadhaa, haipaswi kuwa omba omba duniani na wananchi wake kuishi kwenye lindi la umaskini kama ilivyo sasa, simanjiro ikiwamo" alisema.
Kada huyo wa chadema hivi sasa anatumia muda mwingi kuzunguka sehemu mbalimbali nchini katika kampeni ya chadema ya vuguvugu la mabadiliko (M4C)
Kuhusu uwezeshaji wa kiuchumi wananchi wa wilaya ya simanjiro ambao ni wafugaji, Millya alisema atatumia nafasi yake kuboresha mazingira ua ufugaji na elimu kwa watoto wa kike ambao wengi wa jamii ya kifugaji wa kimasai ambao ndo wengi kwa kujenga shule na kuboresha mazingira ya kusomea ikiwemo mabweni kwa watoto wa kike ambao wengi wao huozwa wakiwa na umri mdogo.
Published by Nipashe on 10th September, 2012
Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO