Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Mh Nassari: Mwenge wa Uhuru hauna tija kwa maendeleo ya wananchi

MBUNGE wa Arumeru Mashariki, mkoani Arusha, kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Bw. Joshua Nassari, ameshikilia msimamo wa kupiga marufuku Mwenge wa Uhuru kufika jimboni kwake na kuwataka wananchi kuupuuza akidai hauna tija kwa maendeleo yao.

Aliwataka wananchi jimboni humo wakae mkao wa kula kwani jitihada za kuyatwaa mashamba makubwa yanayomilikiwa na wageni, zinaendelea hivyo wawe wavumilivu.

Bw. Nassari aliyasema hayo mwishoni mwa wiki katika mkutano wa hadhara wa Operesheni Sangara uliofanyika kwenye Kata ya Usa River, wilayani humo.

Aliwaataka wananchi kuupuuza mwenge huo, kutoshiriki kuchangia mchango wowote na kusisitiza kama mtu yeyote atabughudhiwa kutokana na ujio wa mwenge amualifu.

“Sioni sababu ya Mwenge wa Uhuru kukimbizwa maeneo mbalimbali nchini kwani badala ya kuhamasisha maendeleo, umegeuka sehemu ya ufujaji wa fedha za wananchi.

“Hali hii inachangia umaskini wa Taifa na kuhamasiha maovu katika maeneo yote ambayo mwengu huu unalala, nasema hivi, Mwenge wa Uhuru marufuku kufika jimboni kwangu.

“Mtu yeyote ambaye ataombwa mchango kwa ajili ya mwenge muiteni mwizi na mimi nitakuwa wa kwanza kuuzima baada ya kufika jimboni kwangu,” alisema Bw. Nassari.

Aliwataka wananchi hao kuendelea kushiriki shughuli za maendeleo bila kujali itikadi zao kisiasa na kuihadharisha Halmashauri ya Meru kuzingatia maadili ya utendaji kazi na kuacha kuwabughudhi wananchi kwa kuwachukulia bidhaa zao hasa wanapokusanya ushuru sokoni kupitia wakala wao.

Akizungumzia suala la uvamizi wa mashamba, Bw. Nassari

aliwataka wananchi kuwa wapole kwani anaandaa mkakati wa kuhakikisha ndani ya miaka mitatu, wamiliki wa mashamba hayo wanakimbia wenyewe ili wananchi waweze kujitwalia ardhi yao.

Katika hatua nyingine, Bw. Nassari alisema fedha zilizotengwa na halmashauri kwa maendeleo Kata ya Usa River, kuanzia Julai mosi mwaka huu hadi June mwaka 2013, ni sh. milioni 54.3 ambazo zitatumika kuboresha miundombinu na huduma ya maji safi.

Alisema ukarabati wa barabara kutoka Usa River hadi Magadilishu umetengewa sh. milioni nane na barabara za mji mdogo katika kata hiyo zenye urefu wa kilometa tano, zitagharimu sh. milioni 75.

Katika mkutano huo, wafuasi 15 kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM), na Tanzania Labour Party (TLP) walitangaza kuvihama vyao vyao na kujiunga CHADEMA

ZIFUATAZO NI TASWIRA ZA MATUKIO TOFAUTI YA MKUTANO WA NASSARI ENEO LA TENGERU JANA, ULIOFUATIWA NA ZOEZI LA UFUNGUZI WA MISINGI YA CHAMA KATIKA ENEO HILO. TUNAOMBA RADHI KWA UBORA HAFIFU WA BAADHI YA TASWIRA HIZI

patandi9

patandi8

2012-09-16 18.35.45

2012-09-16 18.35.20

Pichani Mh Nassari akiwasili katika moja ya misingi ya chama kwa ajili ya uzinduzi.

patandi6Kijana Immanuel Saro ambae ni Mwenyekiti wa BAVICHA Wilaya ya Siha akihutubia wananchi wa Tangeru jana.

Patandi4Sehemu ya jukwaa la vijana wa BAVICHA mchanganyiko na wakongwe wengine katika siasa wakifuatilia hotuba mbalimbali katika uwanja wa Patandi eno la Tenegeru jana

patandi3Mwanadada Zion William nae alikuwa na neo la kuzungumza na wananchi. Inawezekana ni mbinu mpya ya CHADEMA kuwajengea uwezo na ujasiri wa kuzungumza vijana wake kwa manufaa ya chama na taifa kwa ujumla, maana idadi kubwa ya wazungumzaji walikuwa vijana wadogo lakini wakitoa maneno yenye hekima ndani yake na kugusa hisia za watu wengi kiasi cha kushangiliwa kila mara

patandiHii ni sehemu ya vijana hao wakiwa wanatabasamu baada ya kuimbishwa wimbo na kada mpya alieahamia chama hicho kutokea CCM mapema mwezi April mwaka huu, Ally Bananga (mwenye kombati nyeusi). Wengine pichani ni Emmanuel Munis kulia kabisa, aliewahi kuwa Mwenyekiti wa Vijana Arusha, Magoma Magona (mwenye Jeans ya bluu katikati) na James Lyatuu, mwenye shati jekundu. Wengine wawili majina yao hayakupatikana mara moja

2012-09-16 18.35.30

Habari imeandikwa na Richard Konga, wa Majira Blog, Arumeru. Picha zote na Frank Oleleshwa

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO