Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Mh Tundu Lissu Afiwa na Baba yake jana

 

Blog hii ilipokea taarifa za msiba jana jioni zikihusu kufariki kwa baba mzazi wa Mh Tundu Lissu  katika hospitali ya Muhimbili, Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Chadema Blog inaelezwa kuwa baba mzazi wa mheshimiwa Tundu Antipas Lissu Mughwai na Mheshimiwa Christina Lissu Mughwai amefariki dunia. Marehemu Augostino Lissu Mughwai (84) alifariki katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa amelazwa akisumbuliwa na maradhi ya moyo kwa muda mrefu.

“the arusha report” inapenda kuchukua nafasi hii kumpa pole Mh Tundu Lissu kwa kufiwa na Baba Mzazi. Tunamtakia ujasiri katika kipindi hiki cha Majonzi na Mwenyezi Mungu amlaze mzee wetu Mahali pema Peponi, Amina

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO