Katika picha tofauti anaonekana Daudi Kilo (mwenye koti la ledha), kamanda wa Chadema kutoka Handeni Tanga akiwa na baadhi ya wanafunzi na walimu wa Shule za Msingi zilizopo katika Wialaya za Karatu na Babati Vijijini baada ya kuwakabidhi zawadi mbali mbali jumla ya wanafunzi 384 waliokuwa wanajiandaa kuanza mitihani ya kumaliza Darasa la saaba mwaka huu.
Daudi Kilo alifanya ziara katika shule za msingi Bashay, Njia Panda, Rhotia na Jushi zilizopo Wilayani Karatu, pamoja na shule ya Tarangire iliyoko babati Vijijini.
Katika ziara hiyo aliambatana na mtu mwingine aliemtambulisha kwa jina la Chris Mbajo, na wote ni wanachama wa Chadema.
Kwa mujibu wa Daudi, aliamua kuwazawadia watoto hao vifaa mbalimbali vya kusomea kwa watoto hao ili kuonesha mapenzi yake kwa Tanzania na namna anavyothamini elimu kwa vijana hasa katika karne hii ya sayansi na teknolojia. Pia kuwaandaa kisaikolojia watoto hao kwa ajili ya mitihani waliyokuwa wafanye kesho yake.
Mbali na ‘lunch box’ hiyo, kila mtoto aliebahatika kupata zawadi za kamanda huyo, alijipatia pia peni, penseli, rula, note book, na ufutio. Pia kulikuwa na ndoo na mabeseni ya kuchotea maji na kunawia. Hii ilifanyika siku moja kabla ya kuanza mitihani yao
0 maoni:
Post a Comment