Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Taarifa: Bodi ya Utalii Tanzania inakuhamasisha kujitokeza kupigia kura vivutio vyote vya Tanzania ili viweze kuwa miongoni mwa maajabu saba ya asili ya bara la Afrika.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

UHAMASISHAJI WA KUPIGIA KURA MLIMA KILIMANJARO, BONDE LA NGORONGORO NA TUKIO LA KUHAMA WANYAMA KATIKA HIFADHI YA SERENGETI KATIKA SHINDANO LA MAAJABU SABA YA ASILI KATIKA BARA LA AFRIKA

 Hivi karibuni pamekuwa na shindano jipya lijulikanalo kama seven Natural Wonders linaloshindanisha vivutio mbalimbali vya asili vinavyopatikana katika kila bara. Shindano hilo linaloendeshwa kwa kupiga kura kupitia tovuti ya http://sevennaturalwonders.org linashindanisha vivutio vya utalii kumi na viwili (12) katika bara la Afrika. Tanzania ni nchi pekee yenye vivutio vingi katika orodha hiyo. Vivutio vya Tanzania ni Mlima Kilimanjaro, Bonde la Ngorongoro, na hifadhi ya Serengeti. Watanzania na watu wote duniani wanahamasishwa kuvipigiakura vivutio hivyo vitatu

Ili kurahisisha upigaji kura kwa vivutio vya Tanzania, Bodi ya Utalii Tanzania imewaomba waandaji wa shindano hilo kuandaa tovuti maalum ambayo ni http://sevennaturalwonders.org/tanzania/ itakayomuhitaji mpigakura kutuma barua pepe yenye kichwa cha habari “TANZANIA” inayoorodhesha vivutio hivyo vitatu (3), na vivutio vingine visivyozidi vinne (4) vilivyopo Tanzania ambavyo mpigakura anaona vinafaa viwemo katika orodha ya maajabu saba ya asili ya Tanzania, kwenda kwenye anuani hii vote@sevennaturalwonders.org. Kwa maelezo zaidi kuhusu vivutio vya utalii Tanzania tembelea www.tanzaniatourism.go.tz.

Shindano  hili linaweza kuwa fursa nzuri kwa Tanzania kujitambulisha pamoja na kuitangazia dunia kuwa Mlima Kilimanjaro, ambao ni mlima mrefu kuliko yote barani Afrika; Hifadhi ya Serengeti, ambapo tukio la kuhama wanyama hutokea kila mwaka; na eneo la Ngorongoro, ambalo ni urithi wa dunia wa asili na utamaduni (natural and cultural World Heritage Site), vyote ni vivutio vilivyopo hapa kwetu Tanzania.
Vivutio vitakavyoshinda vitatangazwa na vyombo mbalimbali vya habari duniani na kupewa hadhi zaidi ya kimataifa.

Tumia fursa hii kupigia kura vivutio vyote vya Tanzania ili viweze kuwa miongoni mwa maajabu saba ya asili ya bara la Afrika.

Imetolewa na Mkurugenzi Mwendeshaji
BODI YA UTALII TANZANIA

mount-kilimanjaroMt Kilimanjaro

nyumbu migration“Nyumbu” migration

Ngorongoro crater

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO