MAHAKAMA ya Haki za Binadamu ya Afrika leo (Jumatatu) inatarajia kuwaapisha majaji wapya wawili, Ben Kioko, kutoka Kenya na El Hadji Guissé kutoka Senegal.
Mbali ya kuapishwa huko, kutafanyika uchaguzi wa rais wa mahakama hiyo pamoja na na makamu wake baada ya rais wa sasa Jaji, Gerard Niyungeko kutoka Burundi na makamu wake Sophia Akuffo wa Ghana kumaliza kipindi chao cha miaka miwili ya uongozi.
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na ofisa habari wa mahakama hiyo, Jean-Pierre Uwanone, hafla hiyo itafanyika kwenye makao makuu ya mahakama hiyo yaliyopo jijini hapa.
Alisema kuwa majaji hao wanaoapishwa waliteuliwa wakati wa mkutano wa 19 wa wakuu wa nchi za Afrika uliokaa Julai 16, mwaka huu, ambapo majaji hao wanatarajiwa kutumikia mahakama hiyo kwa kipindi cha miaka sita.
na Grace Macha, Arusha
0 maoni:
Post a Comment