Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

CCM YASHINDA UCHAGUZI MDOGO JIMBO LA BUBUBU VISIWANI ZANZIBAR.

Chama cha Mapinduzi kimeshinda katika Uchaguzi Mdogo uliofanyika jana katika Jimbo la Bububu kutokana na kifo cha aliekuwa Mwakilishi wa Jimbo hilo Salim Amour Mtondoo.

Akitangaza matokeo Misimaamizi wa Uchaguzi huo Suluhu Ali Rashid amesema kuwa Hussein Ibrahim Makungu wa CCM ameshinda kwa kupata kura 3371 sawa sawa na asilimia 50.7ambapo Issa Khamis Issa wa CUF amepata kura  3204 sawa sawa na asilimia 48.2

Aidha Suluhu amesema kuwa Mgombea wa Chama cha ADC Zuhura Bakari Mohamed amepata kura 45 sawa sawa na asilimia 0.7 wakati Abubakar Hamad Said wa Chama cha AFP amepata kura 8 sawa sawa na asilimia 0.1, Mtumweni Jabir Seif wa Jahazi Asilia amepata kura 7 sawa sawa na asilimia 0.1,Haroun Abdulla Said wa NCCR amepata kura 3 sawa sawa na asilimia 0.0, Suleiman M.Abdulla wa NRA amepata kura 1 sawa sawa na asilimia 0.0 Seif Salim Seif amepata kura tatu sawa sawa na asilimia 0.0 na Juma Metu Domo wa Chama cha SAU amepata kura 4 sawa sawa na asilimia 0.1.

Jumla ya kura 6720 zilipigwa  sawa sawa na asilimia 68.6.Kura 74 ziliharibika sawa sawa na asilimia 1.1Kura halali ziliozopigwa zilikuwa 6646  sawa sawa na asilimia 98.9na waliojiandikisha walikuwa 9799

Source: Mo Blog

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO