Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

CUF wako tayari mjini Arusha kupambana na CHADEMA

cuf ArushaPichani gari la matangazo la chama cha CUF likiwa limeegeshwa katika moja ya mitaa ya Jiji la Arusha tayari kuanza mchakamchaka maalumu uliozinduliwa na Mwenyekiti wa chama hicho taifa, Prof Lipumba tarehe 9 mwezi huu katika viwanja vya Jangwani, Dar es Salaam na kuahidi kupambana na Chadema ili kuvunja ngome zao katika mikoa sita nchini wakianza na Arusha.

Katika Mkutano huo wa Jangwani Makamu Mwenyekiti wa CUF, Machano Hamis Ally, aliwaomba Waislamu wote nchini kujiunga na chama hicho kwa kuwa vyama vingine vinasema ni cha Waislamu.

“Imeelezwa kuwa CCM na CHADEMA wanasema CUF ni chama cha Waislamu basi kama ni hivyo Waislamu wote waingie CUF kwa kuwa vyama vingine hawawataki nyie,” alisema Ally siku hiyo akihutubia.

Aidha katika hali inayoonekana dhahiri kuwa Waislamu hao wameitikia wito wa Makamu Mwenyekiti, Machano Ally kuwataka wajiunge na CUF, tayari kuna jitihada za wazi mjini hapa zikionesha namna ambavyo nyumba za ibada zinavyotumika kufanya siasa.

Hali hii isipodhibitiwa mapema inaweza kuja kuliingiza taifa katika chuki kubwa za kiimani na pengine hata kuwa uadui wa vita.

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

1 maoni:

Anonymous said...

Prettу niсе pοst. Ι just stumbled upon yоur weblog anԁ wanteԁ to say
that I've truly enjoyed browsing your blog posts. In any case I will be subscribing to your rss feed and I hope you write again very soon!
Visit my blog post ... http://www.vapornine.com

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO