Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

MAADHIMISHO YA WIKI YA NENDA KWA USALAMA BARABARANI KUANZA LEO KITAIFA MKOANI IRINGA

Kamanda mkuu kikosi cha usalama barabarani Mohamedi mpinga (Kushoto)  akipokea Tshirt kutoka kwa Afisa Uhusiano wa Airtel Jane Matinde zitakazotumika katika maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani inayofanyika kitaifa mkoni Iringa ambapo Airtel ni wadhani wakuu. Makabithiano hayo yalifanyika katika ofisi za makao makuu ya polisi usalama barabarani jijini Dar es saalam,akishuhudia ni Mkaguzi msaidizi wa polisi Inspector  Deus Sokoni, madhimisho ya wiki ya Usalama barabarani yanaanza leo  jumatatu.


*********

Maadhimisho hayo kitaifa yanafanyika mkoani Iringa viwanja vya Samora
Airtel yakabidhi Fulana zenye Ujumbe maalum kwaajili ya kuhamasisha usalama barabarani

KAMPUNI ya simu za mikononi ya Airtel imeendeleza dhamira yake ya kushirikiiana na jeshi la polisi usalama barabarani katika kuhakikisha ajali za barabarani zinapungua na kudhibitiwa.

Wiki ya nenda kwa usalama barabarani inafunguliwa  kitaifa  mkoani Iringa katika viwanja vya Samora kuanzia tarehe 17-22 mwezi Septemba ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa WAZIRI WA MAMBO YA NDANI MHE. DKT. EMMANUEL NCHIMBI kwa niaba ya Mh, Raisi Jakaya Mrisho Kikwete

Akizungumza na wakati wa hafla maalum ya makabidhiano ya Fulana Ofisa Uhusiano wa Airtel Jane Matinde alisema "Airtel tunaona ni haki na ni sawa kuendelea kuthamini usalama barabarni na tunayo dhamira thabiti ya kuhakikisha tunaelimisha na kuhamasisha jamii na waendesha vyombo vya moto kuzingatia na kutii sheria za usalam barabarani, hivyo basi tunaomba watanzania kuunga mkono jitihada hizi ili kuhakikisha kwamba vyombo vya moto zinakaguliwa na kubandikwa stika maalumu za nenda kwa usalama barabarani"

Airtel inadhamini kampeni hii kwa miaka 4 mfululizo ambapo mwaka huu mbali na kuchapisha stickers imejitolea fulana 800 zenye thamani ya Tsh 8 zilizo na ujumbe maalumu kwa mwaka huu usemao“ Pambana na ajali za barabarani kwa vitendo, zingatia sheria”  makabidhiano hayo yamefanyika katika ofisi za makao makuu ya polisi usalama barabarini jijini Dar es saalam.

"Airtel Tanzania imeamua kuunga mkono kampeni hii ya nenda kwa usalama barabarani kwa sababu ya ongezeko kubwa la ajali za barabarani ambazo zinaathiri wateja wetu, aliongeza Bi Mtinde

Bado Airtel haitaishia hapo tayari tumeshajipanga kufanya kampeni mbalimbali zitakazokuwa zikitoa elimu kwa watumiaji wa barabara hasa waenda kwa miguu na madereva wa vyombo vya moto kwa lengo la kupunguza ajali barabarani huku tukishirikiana na jeshi la polisi usalama barabarani. alimaliza kwa kusema

Nae kamanda Mkuu wa Usalama Barabarani Mohamedi Mpinga alisema "Ninawashukuru sana Airtel kwa ushirikiano wenu katika mkakati wetu wa kupunguza ajali barabarani, hadi sasa maandalizi yote ya wiki ya nenda kwa usalama yamekaa sawa na nawahamasisha sana wananchi wote wajitokeze katika vituo vyetu vyote nchini ili waweze kukagua magari yao na kujipatia stika za usalama barabarani.

Kwa mkoa wa Iringa ambapo ndiko tunafanya maadhimisho ya Usalama barabarani pia tutafanyia ukaguzi pale katika viwanja vya Samora vilevile  kituo cha polisi kati maeneo ya sokoni, kituo cha checkpoint ivumbilo na kile cha mafinga,  alimaliza kwa kusema Kamanda Mpinga.

KWA HISANI YA FADHER KIDEVU

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO