Nyuma ya jengo hilo lilivyovunjwa na vibaya sehemuambayo walikuwa wakiishi watu
Hapa ni ndani ya ofisi ya CUF ambayo ilinusurika kuvunjwa
Kulia ni mwenyekiti wa mtaa(CCM) Mohamed Ali akito ufafanuzi baada ya kutuhumiwa kuwa ameshiriki kufanikisha zoezi hilo la bomoabomoa kushoto aliyevalia shati la CUF ni Naibu Mkurugenzi wa siasa,habari na uenezi Abdal Kambaya
Ofisi za chama cha wananchi CUF wilaya ya Arusha imezuka tafrani ya sintofahamu baada ya jengo hilo kuvunjwa na watu wanaodaiwa kuwa ni majembe huku watu waliokuwa wakiishi ndani ya jengo hilo wasijue pakwenda kutokana na bomoa bomoa hiyo
Tukio hilo la bomoa bomoa lilianza majira ya saa kumi na mbili jioni ambapo taarifa zilitapakaa kwa wananchi kuwa ofisi za CUF zimeungua moto jamba ambalo lilifanya umati mkubwa wa watu kujitokeza kwa wingi
Nyumba hiyo imefikiwa kuvunja kutokana na amri halali ya Mahakama kuu kanda ya Arusha kutoa agizo la kuvunjwa huku tukio hili likihusishwa na maswala ya kisiasa ambapo ofisi ya chama hicho kilinusurika kubomolewa
Wapangaji wa nyumba hiyo walihoji ni serikali gani inaruhusu jengo kuvujwa siku ya jumamosi septemba 29,,pamoja na kuhoji pia waliwalalamikia wanaoshiriki zoezi la kubomoa kuwa wamesababisha kuuibiwa kwa vitu vyao pamoja na fedha zilizokuwa ndani ya nyumba
Viongozi wa CUF wamelaani kuvunjwa kwa ofisi zao kwa kuwa hawakupewa notice ya kuondoka katika jengo hilo
Akizungumzia kwa uchungu Naibu Mkurugenzi na siasa,habari na uwenezi Bw.Abdala Kambaya alisema kuwa tukio hilo lilihusishwa na siasa ambapo wanamtuhumu mwenyekiti na serikali ya CCM
Tukio hilo limejitokea wakati katibu mkuu wa chama hicho CUF ,Mh.Maalim Seif Sharif pamoja na viongozi wengine wa kitaifa wa chama hicho wakiwa tayari wamewasili jijini Arusha kwaajili ya mkutano wa hadhara
Hata hivyo hadi Jamii Blog inaondoka katika ofisi za CUF zilizopo kata ya Kaloleni ulinzi wa askari pamoja na wafuasi wa chama hicho walikuwa makini kulinda ofisi ya chama hicho kisivamiwe
Taarifa za ndani zinasema kuwa zoezi la bomoabomoa litaendelea asubuhi huku Mh.Maalim Seif akitarajiwa kufika katika ofisi hizo kwaajili ya kuweka saini,,,Je atasaini kitabu cha wageni barabarani?
Published by Pamela Mollel on September 29, 2012
1 maoni:
Huyo Mwenyekiti wa CCM Mohamed Ali Mkindi hana jipya hiyo ni familia potofu kwani baba zao walijenga majumba kwa kuiba matofali ya msikiti. hivyo kutumika kwa jambo la kuvunja nyumba hiyo haishangazi,kwani kwanza nyumba hiyo ina kesi ya dhuluma ya matajiri wa mji huo ambao hufanya watakavyo. Watoto wa marehemu wamedhulumiwa nyumba hiyo kwa ushirikiano wa matajiri,mawakili,na mah....na map..... MUNGU ATAWALANI WOTE. KWANI FAMILIA YA MKINDI HAMJIPIMI MUNGU ANAVYOWAADHIBU?
Post a Comment