Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Lissu (Mb): Sababu za CHADEMA kuikataa tume iliyoundwa kuchunguza kifo cha Mwangosi

Alichosema Lissu wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana:
Naomba nianze kwanza kwa kuwapa pole ndugu waandishi wa habari, na wote ambao mko katika kazi hii kubwa ya uandishi wa habari kwa msiba mkubwa ambao, umewapateni kwa kuuliwa mwenzenu, marehemu David Mwangosi.

Kwavile, Mwangosi ameauwa, kwavile tangu jana tunaambiwa kuna tume imeundwa kuchunguza mauaji ya Mwangosi... na vilevile kwa sababu moja ya magazeti yanayoheshimika hapa nchini, leo limehoji kwenye kichwa cha mbele cha habari kwamba, HII TUME, INAWEZA IKAFANYA HAKI? Nazungumzia banner headline ya kwenye gazeti la The Guardian la leo...kwa hiyo naomba kwenye mkutano huu na waandishi wa habari, tuzungumzie hii tume iliyoundwa na Waziri wa Mambo ya ndani, Dk. Nchimbi... na tuone ni kitu gani kinaendelea hapo.

Read more….

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO