Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Eneo wazi la NMC Unga Ltd Arusha lazungushiwa uzio, Chadema kufanyia wapi mikutano yao??

DSC00465

DSC00464Picha ya kwanza na yapili ikionesha nguzo za chuma amabazo zimechimbiwa eneo hilo jana jioni. Blog hii inafuatilia wahusika ili kujua mpango wa matumizi mbadala ya eno hilo la wazi na utafahamishwa hapa hapa.

Kwa usiku wa jana kulikuwa na tetesi zilizozagaa miongoni mwa wakazi wa Arusha hususani wapenzi wa Chadema na kwenye mitandao ya kijamii kuwa uharaka wa kuweka uzio huo ulisimamia na Meya wa Manispaa na Mkuu wa Wilaya ya Arusha kwa kilichoelezwa kuwa ni mkakati wa kuwahujumu Chadema ambao waliomba kufanya mkutano wao leo katika eneo hilo. Pamoja na nguzo hizo kuwekwa hiyo jana, bado kuna shughuli zingine za ujenzi wa mtaro mkubwa wa maji zinaendelea katika eno hilo.

Kwa miaka ya karibuni eneo hilo limejizoelea umaarufu mkubwa kiasi cha kubatizwa “CHADEMA SQUARE” kutokana kuwa sehemu muhimu kwa makutanio ya shughuli nyingi za chama hicho.

DSC00474Kamera yetu ilifanikiwa kunasa magari yakisombea vifusi vya udongo eneo hilo mapema alfajiri ya leo.

DSC00467Huu ndio mtaro wa maji unaoendelea kujengwa pembezoni mwa uwanja huo.

DSC00469Mafungu ya kifusi kilichomwagwa uwanjani hapo kabla ya kusambazwa

DSC00476Karakana ya kimekanika iliyopakana na uwanja huo.

DSC00463Picha hii ilipigwa jana usiku baada ya Blog hii kupata tetesi za kuwako ujenzi wa nguzo hizo kuzunguka eneo hilo kwa lengo.

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO