Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

RAIS KIKWETE ATUNUKIWA TUZO YA UONGOZI BORA KATIKA SERA ZA KILIMO NA CHAKULA

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikabidhiwa Tuzo ya Uongozi Bora wa sera ya Kilimo na Chakula toka kwa Bw. Ajay VAshee, Makamu Mwenyekiti wa asasi isiyo ya kiserikali inayohusika na sera za kilimo na chakula na Maliasili n ijulikanayo kama Food, Agriculture and Natural Resources Policy (FANRPAN) katika hoteli ya White Sands jana Septemba 5, 2012.

Anayeshuhudia kulia ni Katibu Mtendaji wa FANRPAN) Dkt Lindiwe Sibanda. Tuzo hiyo, ambayo hutolewa kwa kiongozi aliyefanya juhudi kuhakikisha kuwepo kwa sera bora za kilimo na chakula nchini kwake, ilichukuliwa na Malkia Ntombi Indlovukazi wa Swaziland mwaka jana, wakati Rais Hifikepunye Pohamba alitunukiwa mwaka 2010, Rais Armando Emilio Gwebuza mwaka 2009 na Rais wa Malawi, Hayati Bingu Wa Mutharika, aliipokea mwaka 2008.

Source: http://francisgodwin.blogspot.com

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO