Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

MCHINA MBARONI KWA KUCHIMBA MADINI KWENYE PORI LA AKIBA LA LWAFI WILAYANI NKASI

Mtambo wa kuchimbia madini ambao Raia wa China walikamatwa wakiutumia katika pori la Akiba la Lwafi wilayani Nkansi kinyume cha sheria.Raia huyu wa china amehukumiwa kulipa faini na kuamriwa kuondoa mtambo huo katika pori hilo.

Baadhi ya raia wa China na Watanzania wakishirikiana kuchimba madini katika pori la Akiba la Lwafi,wilayani Nkansi kinyume cha sheria,ambapo raia hao wa china walifikishwa mahakamani na kuhukumiwa kulipa faini.Picha naTabu Ndziku

--

Na Veronica Kazimoto-Maelezo-Dar es Salaam

Mkurugenzi wa Kampuni ya REDore Mining mwenye asili ya Asia Chaoxian Zhou amehukumiwa kwenda jela miaka minne au kulipa faini jumla ya Shilingi 1,350,000/= kwa kukutwa na makosa mbalimbali likiwemo lakuchimba madini ndani ya hifadhi ya Pori la Akiba la Lwafi wilayani Nkasi kinyume cha sheria .

Kwa mujibu wa taarifa ya Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wanyama pori Paul Sarakikya, mtuhumiwa amelipa faini na kuachiwa huru.Makosa megine aliyopatikana nayo ni pamoja na kuingia ndani ya Pori la Akiba Lwafi kinyume na Sheria ya Kuhifadhi Wanyamapori Na 5 ya mwaka 2009 kifungu  cha 15 na kuharibu mimea ndani ya Pori la Akiba kwa kukiuka kifungu cha 18 cha Sheria ya Kuhifadhi Wanyamapori.

Makosa mengine ni pamoja na kuchimba madini ndani ya Pori la Akiba bila kibali kinyume na Kifungu cha 20 cha Sheria ya Kuhifadhi Wanyamapori na kuchimba madini ndani ya hifadhi kinyume na kifungu cha 95(1) (c) cha Sheria ya madini Na. 14 ya mwaka 2010.

Mshtakiwa alikiri makosa yote mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi Richard Kasele na Mwendesha Mashtaka Bwana Prosper Rwegerera na kupatikana na hatia ya kuchimba madini katika eneo la Kanyamakaa lililoko katika Wilaya ya Nkasi kinyume cha sheria ya Kuhifadhi wanyamapori namba 5 ya mwaka 2009.

Taarifa hiyo imefafanua kuwa mshitakiwa ameamriwa kuondoa mitambo iliyokutwa ndani ya Pori la Akiba la Lwafi na kufukia mashimo na mitaro yote iliyochimbwa kutokana na shughuli za Kampuni hiyo ndani ya siku saba. Aidha Madini yaliyokuwa yamechimbwa katika eneo hilo ambayo thamani yake bado haijajulikana yametaifishwa na Serikali.

Chaoxian Zhou na mwenzake Wei Lyu ambao wote ni raia wa China walikamtwa Julai 25, 2012 ambapo iligundulika kuwa Wei Lyu hakuwahi kwenda mkoani Katavi wala katika Hifadhi hiyo ya Lwafi na kuchimba madini hivyo aliachiwa huru.

SOURCE: HAKI NGOWI

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO