Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

CUF WAKANUSHA MADAI KUWAIGA CHADEMA

Julius Mtatiro

Kuna mwandishi ameniuliza ati CUF kuzindua V4C tumewaiga CHADEMA. Nimemjulisha kuwa amepoteza kumbukumbu na nikamkumbusha kuwa DIRA YA MABADILIKO YA CUF yaani VISION FOR CHANGE au V4C ni vuguvugu lililozinduliwa mwaka 2010.

Nikamkumbusha kuwa wenzetu wamezindua kwa mara ya kwanza MOVEMENT FOR CHANGE au M4C mwaka 2012, nikamwambia nani kamuiga mwenzake?
Jambo la mwisho nililomjulisha ni kuwa CUF kuzindua V4C na kuendeleza ujumbe wa mabadiliko na CHADEMA kuzindua M4C kwa malengo hayohayo ni utaratibuwa kawaida tu kuuandaa umma kutokukichagua CCM mwaka 2014.

Baadhi ya Vyombo vya habari viache chokochoko na kutaka kudanganya baadhi ya vyama ati vimeshashika dola. CUF na CHADEMA kwa huku bara bado ni wapinzani tu, hata kama tukijidai hatujuani, hata kama tukipeana majina mapya ya ujanja ujanja, ukweli ni kuwa CCM ndiyo wanaongoza dola huku bara na tukishangaa wananchi wataendelea kuumia chini ya mikono ya CCM.karibu audiface jackson blogspot kupata habari kila saa..Juhudi za kila chama kujipanga na kuchukua viti zaidi BUNGENI, KWENYE MABARAZA YA MADIWANI, VIJIJI, VITONGOZI NA MITAA, na kupata kura zaidi ndiyo njia ya pekee tuliyonayo hivi sasa baada ya ile ya ushirikiano kushindikana.

Vyama vijipange zaidi na tusipoteze muda wa kutafuta nani kamuiga nani. Siku zote CUF huigwa

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO