Chama cha Wanahabari Wanawake (TAMWA) kimepata Mkurugenzi Mtendaji mpya ambae anachukua nafasi ya Ananilea Nkya aliemaliza muda wake baada ya kutumikia taasisi hiyo kwa miaka kumi na moja.
Mkurugenzi huyo mpya, Valerie Msoka ambae ni miongoni mwa wanahabari wanawake 12 waanzilishi wa TAMWA amefanya kazi za kutukuka katika ngazi ya kitaifa, kikanda na kimataifa.
Valirie alikabidhiwa ofisi jana Alhamis Septemba 27, 2012 katika sherehe fupi iliyofanyika ofisi za TAMWA zilizopo Sinza Mori, Dar es Salaam.
Valerie aliwahi kufanya kazi Redio Tanzania, BBC idhaa ya Kiswahili na Kiingereza kabla ya kujiunga na umoja wa mataifa.
Valerie ana shahada ya Uzamili katika fani ya uandishi wa habari kimataifa (M>A International Journalism) kutoka Chuo Kikuu cha City nchini Uingereza, na amefanya kazi maeneo yenye vita kama Sudan, Iraq, Rwanda, Congo na Burundi.
0 maoni:
Post a Comment