Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Mwanaume achunwa ngozi Iringa

achunwa ngoziTukio la kusikitisha limetokea katika Kijiji cha Wenda Lutongoji cha Lupeta, Iringa ambapo mwili wa mwanakijiji aliyetambulika kwa jina la Leornad Kutika (49) umekutwa katika nyumba aliyokuwa akiishi huku ukiwa umechunwa ngozi, kunyofolewa macho pamoja na kukatwa sehemu za siri.

Baba mdogo wa marehemu Martin Kutika, mkazi wa Lupeta anaeleza kuwa usiku wa kuamkia jana alipigiwa simu na ndugu wa marehemu aliyefahamika kwa jina Kibadeni Kutika kuwa ndugu yake huyo ambayekwa mujibu wa maeezo yake alikuwa akisumbuliwa na tatizo la akili alikutwa katika nyumba aliyokuwa anaishi huku akiwa amefariki na kuondolewa sehemu za siri na kuchunwa ngozi.

Marehemu anaelezwa kuwa alianza kusumbuliwa na tatizo la kurukwa akili tangu alipokuwa mdogo japo hakuwahi kufanya vurugu yoyote na wao kama familia wamekuwa wakimpatia chakula na siku mbili kabla ya tukio marehemu alionekana lakini baada ya hapo hawakumuona tenda ndipo wifi yake alipofika nakukuta marehemu amekufa huku akiwa ametendewa unyama huo. Pichani ni nyumba alimokutwa marehemu.

Taarifa hii ni kwa hisani ya Francis Godwin Blog, Iringa. Tunaomba radhi kwa picha hii ya kutisha

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO