Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Zanzibar kuwa makao makuu ya kamisheni mpya ya lugha ya Kiswahili

Jumuiya ya Afrika Mashariki imepitisha kwa kauli moja Zanzibar kuwa makao makuu ya kamisheni mpya ya lugha ya kiswahili ambayo itazinduliwa hivi karibuni.
Kamishna wa Utamaduni Zanzibar Hamad Bakar Mshindo (kulia) akitoa maelezo ya Jengo hilo ambalo ndio Makao makuu ya Jumuiya ya Kamisheni ya Kiswahili ya Afrika Mashariki Mkutano Wa Jumuiya Ya Kamisheni Ya Kiswahili Afrika Mashariki Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni Wizara ya Habari,Vijana na Utamaduni Tanzania  Profesa Hermas Mwansoko akitoa maelekezo kwa wajumbe wa Jumuiya  Kamisheni ya Kiswahili ya Afrika Mashariki

Taarifa ya Miza Kona, wa Maelezo Zanzibar inaeleza zaidi…

Kuwepo kwa Makao makuu ya Kamisheni ya Kiswahili ya Jumuiya ya Afrika Mashariki mjini Zanzibar kutasaidia kukuza Lugha ya Kiswahili,Utamaduni na Michezo kwa nchi wanachama wa Jumuiya hiyo. Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni Tanzania Profesa Hermas Mwansoko katika ukumbi wa Eacrotanal wakati walipokuwa wakijadili uanzishwaji wa Makao makuu ya kamisheni ya Kiswahili ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na kuangalia Itifaki ya kuanzisha Kamisheni ya Utamaduni na Michezo.

Amesema kuwa Zanzibar ni chimbuko la Kiswahili sanifu hivyo ni vyema kuirejesha historia ya kiswahili hapa nchini ili kiweze kukuwa zaidi na kuwepo muendelezo mzuri wa lugha, utamaduni na michezo kwa nchi wanachama wa jumuiya hiyo. Aidha Profesa Mwansoko amesema kuanzishwa kwa jumuiya hiyo Zanzibar kutatoa nafasi za ajira kwa wazanzibari wenyewe kwani wataweza kupata ajira na kuweza kutoa wataalamu wazuri wa lugha ya Kiswahili jambo ambalo litapelekea maendeleo nchini. Amefahamisha kuwa, kuwepo kwa makao makuu hayo hapa nchini kutaweza kudumisha mashirikano ya karibu kwa wanachama wa Afrika Mashariki katika mambo ya utamaduni na michezo.

Aidha alisema lengo la mkuutano huo ni kuleta wataalamu wa lugha na utamaduni ili kuweza kujadili kuhusu utamaduni na michezo katika nchi za Jumuiya Afrika ya Mashariki ambazo zitaweza kukuza utamaduni wake na kujipatia maendeleo na kuepukana na umasikini katika nchi hizo. Akielezea kuhusu mijadala Profesa Mwansoko amesema kuwa Jumuiya hiyo itajadili marekebisho ya uanzishwaji wa kamisheni ya Utamaduni na michezo na kuweza kufikia lengo iliyojiwekea jumuiya hiyo.

Kwa upande wao washiriki wa Mkutano huo wameishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa ushirikiano wao na kuweza kukubali Makao makuu ya Kamisheni hiyo kuwepo Zanzibar na kutoa fursa nzuri ya kukikuza kiswahi katika nchi za Afrika ya Mashariki. Jumuiya hiyo itakuwa na makao makuu yake hapo Eacrotanal mjini Zanzibar ambapo wanachama wote kwa pamoja walikubaliana na kuridhika kuwepo kwa makao makuu hayo katika eneo bila pingamizi yoyote. Mkutano huo wa wiki moja ambao utajadili mada mbalimbali zinazohusiana na utamaduni, michezo na lugha ambao umewashirikisha wanachama kutoka Burundi, Kenya, Uganda, Rwanda na Tanzania.

Picha kwa hisani ya Mjengwa Blog

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO