Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Breaking News: Machinga Arusha wavamia eneo lililouzwa kifisadi na kujigawia kwa biashara zao, Polisi wakacha kutumia mabomu kuwatawanya

vurugu machinga arushaWakati wakibomoa uzio hali ilikuwa hivi… (picha hii ni kwa hisani ya Saimon Frank, na the Moment of Truth Blog)

DSCN5279Pichani, wananchi wa Arusha (wafanyabiashara ndogo ndogo maarufu kama machinga) wamama, wababa, na vvijana wakionekana kujigawia vijisehemu vya kufanyia biashara mapema leo asubuhi baada ya kufanikiwa kuvamia eneo lililo jirani na soko la Kilombero na kuvunja uzio.

Hatua hiyo inaelezwa ilichangiwa na kitendo cha Manispaa kuwaondoa wafanyabiashara wote waliokuwa wakifanya shughuli zao nje ya soko la Kilombero ambao walielezwa kuwa walipaswa kuhamia eneo jipya la NMC Unga Ltd.

Kwa mujibu wa maelezo ya baadhi ya machinga waliozungumza na Blog hii wanasema kilichowakasirisha na kuamua kuvamia eneo hilo na kujigawia maeneo ni kitendo cha mgambo wa manispaa kuwakamata asubuhi ya leo na kuwatoza faini ya elfu 50 huku wakitakiwa waondoke maeneo ya nje ya soko na kuhamia NMC ambako wamedai tayari kumejaa.

Blog hii iliweza kushuhudia umati wa watu ambao kimsingi hawawezi kueneo eneo jipya la NMC walikogawiwa hivi karibuni ambako tayari kuna vibanda kiasi cha watu wengi kufanyia biashara zao nje ya uzio uliowekwa!

Eeno lililovamiwa hii leo linaelezwa kuwa na mgogoro wa muda mrefu kati ya Manispaa na mmiliki wake ambae anaelezwa kutokuwa mmiliki halali na kwamba liliuzwa kifisadi na kwa ushirikiano na Meya wa Manispaa aliyepita.

DSCN5306

DSCN5307

DSCN5264Vikosi vya askari Polisi vikiwa tayari tayari kiulinzi. Tangia kuanza kwa zoezi la uvamizi Polisi hawa walikuwa pembeni wakiangalia vurumai hizo bila kuwazuia wananchi hao walioonekana kuwa wengi sana, wenye hasira na umoja. Pengine ni busara imetumika na jeshi la Polisi kuepusha vurugu kuwa na madhara zaidi.

DSCN5296 DSCN5262Waandishi wa habari na mashuhuda wengine wakishangaa tukio lilivyokuwa

DSCN5275Kila mtu yuko bize kuwahi kijieneo chake

DSCN5277

DSCN5285Baadhi ya sehemu katika eneo hilo zilikuwa tayari zimeendelezwa kwa kuanza ujenzi wa jengo la ghorofa, ujenzi ambao unaelezwa kusimamishwa na Mahakama siku za nyuma.

DSCN5279

DSCN5293Kamba zimewekwa kuonesha mipaka ya kila mtu

DSCN5294Kina mama hwakuwa nyuma nao kujimegea vijisehemu

DSCN5278

DSCN5302Matairi yaliyochomwa moto yakiendelea kuteketea

DSCN5301

DSCN5314

DSCN5310

DSCN5311

DSCN5313Picha nne za mwisho ni eneo jipya la machinga, NMC ambako tayari kumejaa kama picha zinavyoonesha mabanda na kina mama wakifanyia biashara zao nje ya uzio. Ni takribani wki moja tu tnagu machinga waruhusiwe kutumia eneo hilo. Picha zote na Tumainiel Seria

Blog hii itanendele kufuatilia hatma ya mgogoro huu na kukujuza.. endelea kutembelea hapa!!

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

2 maoni:

Anonymous said...

My Town Chezea Ar Hakunaga

Charles Nazi said...

Kitabu cha mbinu za biashara kwa email

Napenda kuwaarifu kwamba sasa, kitabu cha mbinu za biashara na maarifa ya kupata pesa na utajiri, unaweza kukipata kwenye email yako kwa mfumo wa PDF. Kwa wale wanaohitaji wanaweza kunitumia Sh. 5,000 kwa M PESA kwenye simu namba 0755394701 kisha kunitumia email zao na mimi nitawatumia email iliyoambatanishwa na kitabu.

Kitabu hiki kinalenga kumsaidia mtu yeyote ambaye anatafuta utajiri kwa kufanya biashara ndogondogo hadi kubwa. Pia kinatoa maarifa, mbinu na mikakati mbalimbali ya kupambana na umaskini, kinatoa elimu ya biashara na mbinu mbalimbali za namna ya kupata pesa kwa njia halali ili kukurahisishia safari yako ya kuelekea kwenye kutafuta na kupata utajiri. Kitabu hiki kina sehemu mbili, sehemu ya kwanza inaeleza kuhusu taratibu za kuanzisha biashara sheria, utafiti wa masoko, utunzaji wa hesabu za biashara na utatuzi wa matatizo ya biashara. Sehemu ya pili inaelezea kuhusu mawazo, mbinu mbalimbali za biashara unazoweza kuzifanya na kupata faida na hivyo kutajirika.
CHARLES NAZI
http://www.squidoo.com/kitabu-mbinu-za-biashara

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO