Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Ufafanuzi wa kilichotokea Uchaguzi Wa Meya Mwanza.

CCM wameshindishwa na mbinu za kisiasa ambazo uhalali wake kisheria linabaki kuwa suala la wanasheria wanaojua taratiu zikoje.

Baada ya mgawanyo wa h/shauri ya jiji na kuwa na h/shauri ya jiji inayoundwa na jimbo la Nyamagana na halmashauri ya ilemela inayondwa na jimbo la ilemela mwezi Julai mwaka huu mgawanyo wa madiwai ulikuwa hivi kwa

Nyamagana

  1. Chadema -wa kata 5, viti ,maalum 2. mbunge mmoja, jumla wanakuwa 8
  2. CCM – wa kata 6, viti maalum 1 jumla wanakuwa 7
  3. Cuf – wa kata 1, viti maalum 1

Ilemela

  1. Chadema — wa kata 6, viti maalum 2 mbunge 1 jumla wanakuwa 9
  2. CCM – wa kata 3, viti maalum 2 na mbunge 1 (wa viti maalum) jumla wanakuwa 6
  3. CUF – MBUNGE WA viti maalum 1

Kilchotokea kwenye uchaguzi ni CCM kuhamisha diwani mmoja wa viti maalum (kwa barua ya CCM kwenda kwa mkurugenzi wa jiji ya tarehe 14, Septemba, 2012) na mbunge wa viti maalum toka Ilemela kuja nyamagana na hivyo kuongeza idadi ya kura zao kuwa 9, wakati huo huo Chadema walishakuwa hawaihehabu kura ya Diwani wa Igoma Chagulani ambaye wamemfukuza uanachama akalejeshewa na mahakama wao wanapugukiwa na kura 1 zao zinabaki 7 , aliyepungua Chadema akiwapigia CCM wanakuwa na kura 10 dhid ya 7 za Chadema.

Lakini pia CUF walishakubaliana na chadema kuungana mkono, kwa hiyo kwa kura 2 za CUF Chadema wangekuwa na kura 9, lakini inaonekana ama mwana Chadema mmoja kapigia CCM au CUF mmoja kapigia CCM na kufanya matokeo ya kuwa kuwa 11 kwa CCM dhidi ya nane za Chadema.

Hiyo ndiyo hali halisi ya jinsi mahesau ya kura yalivyochezwa, kama kuna uhalali katika mchakato huo au la ni suala la wataalamu wa masuala haya kutujuza.

Hayo yakiendelea uchaguzi wa Meya wa Ilemela meahirshwa katika mazingira tata, baada ya Mkurugeni kusoma Amri ya Mahakama iliyopewa tafsiri na mwanasheria wa jiji kuwa inakifanya kikao hicho kuahirishwa kwa kuwa Diwani wa Chadema Matata (pia alifukuzwa uanachama pamoja na wa igoma na anaendelea na udiwani kwa amri ya makahama) kuleta pia barua ya kutaka atambuliwe kaa mgombea.

Ukazuka ubishi kidogo juu ya hoja ya mgombea kuteuliwa na chama, mkurugenzi wa jiji akasema hiyo siyo sheria ni mwogozo, na kwa kuwa sheria na mwongozo zikigongana sheria ndiyo inatamalaki hatakia aingie katka mgogoro wa tafsiri ya sheria, akaahirisha kikao bila hata madiwani kujadili hoja hiyo.

Kwa mujibu wa mwanasheria wa  Chadema, pingamizi hilo lilikuwa linawarejeshea haki yao ya uanachama na hivyo kuendelea na udiwani wao, na kutaka matata asizuiliwe kuendelea na mchakato wa kuomba umeya, Kwa hiyo matata ameomba lakini hakuteuliwa na chama na mahakama haiwezi kuwalazmisha chama wateue mgombea kwa amri ya mahakama, anadhani ni uhuni tu na njama za kisiasa zimefanyika kuahirisha uchaguzi huo.
Nadhani kidogo piacha itaeleweka kwa wanjamvi juu ya nini hasa kimetokea.

SOURCE: Kamanda Deus Bugaywa-Mchambuzi Raia Mwema

Ushuhuda wa aliyekuwa eneo la tukio;

Wakuu habari,

Kama inavyojulikana dunia nzima sasa, siasa za Tanzania kwa leo zilikuwa katika Jiji la Mwanza, ambako kulitakiwa kuwa na chaguzi mbili za kuwapata Mameya wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza (Nyamagana) na Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela. Muundo huu mpya unatokana na uamuzi wa serikali ya CCM kuligawanya lililokuwa Jiji la Mwanza katika halmashauri mbili tofauti.

Kabla ya hapo Jiji la Mwanza lilikuwa na muundo wa aina yake nchini. Ilikuwa ni halmashauri pekee iliyokuwa ikihusisha wilaya mbili tofauti, Nyamagana na Ilemela.

Nimeandika ‘kulitakiwa’ kuwa na chaguzi mbili kwa sababu uchaguzi mmoja kutokana na mizengwe iliyotengenezwa na inayoendelea kutengenezwa katika ‘jiji’ la Mwanza.

Wakati madiwani wa Nyamagana (now Jiji la Mwanza), wamepiga kura kumchagua Meya na Naibu Meya wake, uchaguzi wa Ilemela umelala. Wanaotaka kuumiliki uchaguzi huo ili uende wanavyotaka na hatimaye utoe matokeo wanayotaka, wanasema eti umeahirishwa. Ni mwendelezo wa siasa za kihuni zinazofanywa na walioko madarakani.

Mwanza; just another Arusha in the making, asanteni kwa makosa

Baadhi ya vyombo vya habari vya leo (ofcourse magazeti, maana kwa staili ya electronic zetu, hardly unaweza kupata analytical reporting), zilionesha namna ambavyo kulitegemewa kuwepo na mnyukano mkali kuwania kiti cha Umeya na Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza (Nyamagana), kati ya CHADEMA na CCM.

Katika uchaguzi huu ambao ulikuwa unaanza kwa kufanyika asubuhi ya leo, madiwani wa CHADEMA na CCM walikuwa pasu kwa pasu. Huku saba na huku saba. Ofcourse katika hao saba wa CHADEMA, hakuna mtu anaitwa Adams Chagulani, aliyevuliwa uanachama na Kamati Kuu ya Chama karibuni. Hivyo wapiga kura wa CUF, ndiyo walitegemewa kuwa ‘marefarii’. Chama hicho kina madiwani wawili, mmoja wa kuchaguliwa na mwingine wa viti maalum.

Kama yalivyoandika baadhi ya magazeti leo, baada ya kuona hali ya pasu kwa pasu iliyokuwepo, wana uwezekano mkubwa wa kuangukia pua katika nafasi ya umeya, walioko madarakani wakageukia njama na hila. Kinyume na taratibu zilizotumika wakati wa kugawanya halmashauri, wakaongeza wapiga kura wawili kutoka Ilemela, mbunge na diwani mmoja. Idadi yao ikatimu 9.

Wakati huo huo Mkurugenzi wa Jiji, Wilson Kabwe (nafikiri mnamkumbuka vyema), alishamkubali Adams Chagulani kuwa mmoja wa wapiga kura. Unaweza kujumlisha na kujua idadi ya wapiga kura ilifikia wangapi ukiongeza na idadi niliyoitoa kabla. Kwa hila hizo, mpaka hapo mtumbwi ukaanza kutobolewa. Mnaelewa.

Wakati hayo yakifanyika, wananchi wamezuia kabisa kuingia mahali pa uchaguzi. Kinyume na taratibu za uendeshaji wa vikao vya halmashauri. Nje wakaleta gari mbili zimejaa askari. Wako full geared. Kwa hiyo tayari walisha- anticipate kuwa watavuruga na watu hawatakubali. Wakaanza kujihami kwa hila zao.

Kura zikapigwa. Matokeo nidyo kama hayo ambayo watu wengi hapa tayari mnayajua, 11-8. Kuwa honestly, hata kama kura ni siri, haitarajiwi kuwa Chagulani ambaye anapita barabarani akibeza uamuzi wa Kamati Kuu ya CHADEMA na viongozi wa chama, hivyo ana hasira, angeipigia kura CHADEMA. Never. So unaweza kupiga hesabu zako kichwani.

Kwenye nafasi ya Unaibu Meya, ambayo walipambana mgombea wa CCM na CUF, kura zikabadilika kidogo. Ikawa 10 (CCM)-9 (CUF). Hapa unaweza kuona kuwa madiwani karibu wote wa CHADEMA walimpatia mgombea wa CUF hivyo plus kura yake na ile ya diwani mwenzake, zikawa tisa. CCM waka-maintain kura zao na washirika wao

Mpaka hapo kulikuwa na two school of thoughts kwa nini jamaa waliamua kuhamisha wapiga kura wao kutoka Ilemela kwenda Jiji, je ni kwa sababu walidhamiria kuchukua jiji na kuitosa Ilemela au walikuwa wanataka kufanya hila za kusababisha vurugu?

Ilemela

Uchaguzi wa Ilemela ulipangwa ufanyike majira ya saa 9. Ilipofika wakati wa kupiga kura, hila zikaanzishwa na kuzuliwa. Mkurugenzi aliyeruhusu mtu anayeitwa Chagulani apige kura kule Nyamagana, akisema kuna court order/injuction, kufika Ilemela akageuza kibao kuwa amri ya mahakama imezuia kikao hicho kisifanyike. Wakati anajua kabisa kuwa amri iliyopo inahusu watu wawili walioomba mahakama iwalindie udiwani wao kwanza. Yeye akaigeuza kuwa imezuia kikao. Mapema kulikuwa na harakati kubwa zikiongozwa na CCM na mtu mmoja aitwaye Henry Matata, kutaka uchaguzi huo usimamishwe. You see the game!?

Pamoja na madiwani wetu kushinikiza uchaguzi ufanyike, haukufanyika. Na katika uchaguzi huu wa pili, CHADEMA Ilikuwa na absolute majority dhidi ya CCM pamoja na kushinikiza wao. Kama kura zingepigwa for party lines, CCM walikuwa wanaanguka mapema asubuhi. Wakaliona hilo. Wakifanya waliyofanya.

Hapa ikapatikana another school of thought ya kwa nini walihamisha na kubeba wapiga kura kutoka Ilemela kwende Nyamagana. Kupata muda wa kujipanga namna ya kufanya hila.

Tusubiri kesho wanahabari wetu watatujuza mengi mengine, maana tunawategemea katika kupata ukweli aw kilo hakuwa kikijiri chini ya kapeti.

Lakini makosa na hila waliyofanya leo, it gonna be another blessing in disguise. Hii inadhihirisha kuwa Chama Cha Mabwepande they never learn from the past, they can’t make the present and can’t predict the future. It is total failure. Watanzania wanaendelea kushuhudia the failing govt and falling of the state party.

Wanachukua vyeo kwa nguvu, CHADEMA inaendelea kuishi kwenye mioyo ya watu wanayo news, kushuhudia, kunyanyaswa na kunyimwa haki na stahiki zao. It is, we, the people Vs wenye vyeo.

Wananchi wanajua. Wameona na wamesikia. Wanajua who is who in the whole game. Thee know thy enemy. They have only one duty, to stand against all odds, kupigania haki, uwajibikaji na utu wa mwanadamu. Kwa namna hii wataendelea kusimama na CHADEMA dhidi ya wanaofikiri wataweza kuzuia mabadiliko.

Taarifa hii imetoka Jamiiforums kupitia WotePamoja.Com

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO