Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Mdau apinga Airport Mwanza kubadilishwa jina

 

"Nimesikia kusudio la kubadili jina la uwanja wa ndege wa Mwanza kuwa; Serengeti International Airport. Miongoni mwa sababu ya chaguo la jina ikiwa ni kukuza utalii hususan kwa kuitangaza mbuga ya Serengeti".Alisema Dalali (pichani kushoto) katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa facebook.

Uwanja wa ndege wa Mwanza ni moja ya viwanja vikubwa vilivyoko Tanzania ukiacha Kile cha Mwalimu Nyerere International airport cha Dar es salaam,kilimanjaro international airport mkoani kilimanjaro na vile vilivyoko Zanzibar .Kwa muda mrefu serikali imekuwa ikihudumia viwanja vya ndege bila kuwa na mikakati madhubuti ya kuimarisha viwanja hivyo kwa kuwekeza kikamirifu ili kuinua uchumi kupitia viwanja hivyo.

Dalali aliendelea kwa kusema "Kama tumefikia kuwa ni Taifa ambalo hatuweki mikakati madhubuti na tukaisimamia kujiimarisha kiuchumi nk na kutegemea "majina" yatafanya kazi hiyo basi tushagota!
Kama tunaweka "attention" katika vitu vidogo (ingawa haimaanishi havina tija) kama jina kuliko kuangalia kwa upana wake vitu kama uimarishwaji wa miundo mbinu na kuenenda na usasa tunaweza kuona Taifa na tuliowapa ridhaa kutuongoza wanapotufikisha.Kifalsafa hii ni "fallacy".
Na tukijiuliza kwa undani; kuna watalii wangapi wanavutika kutembelea kisa "jina la uwanja", hata sio ubora wa uwanja kulinganisha na wale ambao wanavutwa na vivutio? Kweli watalii wanatafuta jina la uwanja wakati wakisaka vivutio wanavyopenda kutembelea? au vivutio vyenyewe?"
Natamani tungewekeza nguvu, akili na maarifa mengi katika kuangalia utekelezaji wa mbinu na mikakati ya kuimarisha na kuwa na miundo mbinu ya kisasa na imara kuliko namna tunavyowekeza nguvu, akili na maarifa katika kuchagua majina nk.

Pichani ni ndege aina ya Boeing 707-351C ya shirika la ndege la Trans Arabian Air Transport ikiwa imeanguka ndani ya ziwa victoria masaa machache kabla ya kujaribu kutua katika uwanja wa ndege wa Mwanza,tatizo likiwa ni kukoekana kwa umeme katika uwanja huo wa ndege mnamo February mwaka 2000.

Pichani ni ndege ya Air Tanzania iliyoanguka baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa Mwanza

Hii ndiyo sehemu ya kukimbilia ndege (runway )ya uwanja wa ndege wa Mwanza.

Remains of McDonnell Douglas DC-8 at Mwanza Airport, Tanzania

Pichani ni mabaki ya ndege ya McDonnell Douglas DC-8 ikiwa imeanguka baada ya kujaribu kuruka kutoka katika uwanja wa ndege wa Mwanza.

http://mw2.google.com/mw-panoramio/photos/small/1155770.jpg Uwanja wa ndege wa Mwanza ukionekana ukiwa katika hali mbaya sana kiasi cha kuhatarisha hata matumizi ya ndege kiwanjani hapo.

Serikali na wadau wote wa mamlaka ya viwanja vya ndege tuamke na mtazamo wa kukuza viwanja vyetu kwa lengo la kuvutia wawekezaji na kukuza maendeleo ya nchi.

Katika picha ni maji yaliyojaa katika uwanja wa ndege wa Mwanza ,hii inaonyesha ni jinsi gani miundombinu ya uwanja huo isivyo imara kiasi cha kuzuia mafuriko hayo

STORY AND PICTURES: BUSINESS MANUAL

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO