Taarifa za kuaminika zimemnukuu Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Arusha, Bw Amani Golugwa akitangaza kuahirishwa kwa mkutano mkubwa wa kisiasa uliokuwa umepangwa kufanyika leo katika viwanja vya NMC, vilivyoko eneo la Unga Lt Jijini Arusha.
Kwa mujibu wa chanzo cha taarifa, uamuzi wa kuahirisha mkutano huu unafuatia kushindikana kuutumia uwanja huo baada ya kile kinachoelezwa kuwa hujuma za baadhi ya watendaji wa Serikali.
Inaelezwa kuwa kitendo cha Mkurugenzi wa Manispaa kuamua ghafla kuendesha zoezi
la kuandaa eneo hilo kwa ajili ya shughuli za wamachinga wa Jijini hapa ndicho kimesababisha Mkutano huo usiweze kufanyika kwa siku ya leo.
Awali ilielezwa kuwa, kwa siku ya jana hadi usiku kulikuwa na pilika pilika nyingi katika uwanja huo kuzungushia mabomba ya kuweka uzio na kusambaza vifusi kwenye mashimo yaliyo viwanjani hapo, hali iliyotafsiriwa na baadhi ya watu kuwa inaweza kuwa ni mkakati wa kuhujumu mkutano huo usifanyike hapo.
Haijaweza kufahamika mara moja kama zoezi hilo la kubadili matumizi ya uwanja huo lina baraka za baraza la Madiwani ama ulikuwa ni uamuzi wa Mkurugenzi mwenyewe.
Rufaa ya Lema
Katika hatua nyingine, kuna taarifa za wasiwasi kuhusiana na kama rufaa ya Lema kupinga kuvuliwa ubunge wake inaweza kusikilizwa kesho Septemba 20, kama ilivyokuwa imepangwa hapo awali.
Upande wa mrufani (Lema) uliandika barua kwa Msajili wa Mahakama kuomba shauri hilo lisogezwe mbele kutokana na msimba uliompata mmoja wa mawakili wa upande wa walalamikaji, Mh Tundu Lissu aliefiwa na baba yake mzazi wikendi iliyopita!
0 maoni:
Post a Comment