Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

CUF Wapigwa mawe Arusha

“INASIKITISHA SANA - VIONGOZI WETU WAMEJERUHIWA VIBAYA ARUSHA
Pamoja na kutoa tahadhari kubwa kwa viongozi wa polisi Arusha, kuwa wenzetu wa CHADEMA wanapanga kwa nguvu zote kuwaogopesha wananchi wa ARusha wasihudhurie mikutano yetu kwa kupanga kuwapiga na kuwaumiza viongozi na wafuasi wetu, jeshi la polisi halikuchukua hatua yoyote.
Hatimaye dkk chache zilizopita, viongozi na wafuasi wetu wameva
miwa na KUPIGWA SANA KWA MAWE na wafuasi wa CHADEMA walioandaliwa kwa ajili ya kazi hiyo.

Dhahma hii imewakuta viongozi na wafuasi wetu waliotangulia Katika eneo la SOKO LA KILOMBERO kwa ajili ya kuendelea na matangazo ya mkutano wa jumapili.

Mawe yalirushwa kama mvua kuelekea kwa wafuasi wetu bila sababu. Ni marundo ya mawe yaliyokuwa yameandaliwa mahsusi kwa ajili hiyo. Cha kushangaza zaidi ni kuwa HAYA yametendeka mbele ya polisi.
Majeruhi wameshakimbizwa hospitalini.

Tunajua MUNGU yuko kila upande, lakini SIASA za kutafutana kuuana haziwezi kuwasaidia wananchi.
Chama kinawaomba wafuasi wetu mahali popote pale walipo WASILIPIZE KISASI, damu inayomwagwa kimakusudi italipwa kwa mkono wa mungu.

CUF hatutawavizia wanachama na viongozi wa CHADEMA kuwapiga wala kuwaumiza, lakini wakumbuke MALIPO ni hapahapa.”

Hii ni taarifa ya Naibu Katibu Mkuu Bara wa CUF, Julius Mtatiro kupitia mtandao wa Facebook.

Aidha, hapo awali Blog hii ilihabarishwa na vyanzo vyake vya taarifa kuwa wakati vurugu za machinga kuvamia eneo na kujigawia kwa biashara zikiendelea katika eneo la Kilombero mapema leo asubuhi, lilipita gari la matangazo la CUF katika eneo hilo na kuanza kuwatangazia kuwa CUF ni chama dume. Maneno hayo na kejeli nyingine vilisikiwa na wananchi hao waliokuwa na hasira muda huo na kuanza kuhoji kama wao CUF ni chama dume, je chama jike ni kipi? Hakuna uthibitisho kwamba waliowapiga mawe ni wafuasi wa chama cha siasa au ni wananchi tu wenye hasira

Hatua hiyo ilifuata na kuwafukuza CUF kwa mawe kutoka eneo hilo.

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

2 maoni:

Rundugai said...

hiyo tahadhari kweli uliitoa mapema kabisa KISHA watawatupia watu mpira

Anonymous said...

Unajua haya maneno ya Mtatiro ukiyatazama sana unaona ni kama mtu anatafuta mahali pa kutokea. Si haki na halali kabisa kuwasingizia Polisi maana tangu asubuhi Polisi walikuwepo eneo hilo na wasijue cha kufanya kudhibiti wananchi wale waliokuwa na hasira...

Lakini pia kusema kuna mawe yamendaliwa ka ajili hiyo ni uongo mkubwa kwa sababu bila Manispaa kumakka na kuwakimbiza machinga leo waliokuwa nje ya soko wala uvamizi huo usingetokea.. Sasa kama chanzo cha vurugu ni macinga kuondolewa, huyu kiongozi anaetaka jamii imuamini anaweza kuhtibitisha mawe hayo yaliandaliwa lina na wapi? Na je katika zunguka yao ya matangazo waliwahi kupitia njia hiyo hata siku moja au kwa vile leo walikuta mkusanyika wakaona watek advantage..

Kuhusu wananchama wa Chadema walioandaliwa, anauhakika gani kwamba mchainga wale ni wanachama wa chama cha siasa na kwamba walipandwa? kwasababu kwa zaidi ya wiki CUF wako Arusha na hakujawahi tokea tukio la kukwaruzana baina ya CU na watu wengine zaidi ya wananchi kuendelea na shughuli zao na kukataa kuhudhuria! Zaidi wanamsuniri Prof Lipumba arudi nchini...

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO