Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

OFISI ZA CUF ARUSHA ZAKUMBWA NA BOMOA BOMOA

Nyuma ya jengo hilo lilivyovunjwa na vibaya sehemuambayo walikuwa wakiishi watu

Hapa ni ndani ya ofisi ya CUF ambayo ilinusurika kuvunjwa

Kulia ni mwenyekiti wa mtaa(CCM) Mohamed Ali akito ufafanuzi baada ya kutuhumiwa kuwa ameshiriki kufanikisha zoezi hilo la bomoabomoa kushoto aliyevalia shati la CUF ni Naibu Mkurugenzi wa siasa,habari na uenezi Abdal Kambaya

Ofisi za chama cha wananchi CUF wilaya ya Arusha imezuka tafrani ya sintofahamu baada ya jengo hilo kuvunjwa na watu wanaodaiwa kuwa ni majembe huku watu waliokuwa wakiishi ndani ya jengo hilo wasijue pakwenda kutokana na bomoa bomoa hiyo

Tukio hilo la bomoa bomoa lilianza majira ya saa kumi na mbili jioni ambapo taarifa zilitapakaa kwa wananchi  kuwa ofisi za CUF zimeungua moto jamba ambalo lilifanya umati mkubwa wa watu kujitokeza kwa wingi

Nyumba hiyo imefikiwa kuvunja kutokana na amri halali ya Mahakama kuu kanda ya Arusha kutoa agizo la kuvunjwa huku tukio hili likihusishwa na maswala ya  kisiasa ambapo ofisi ya chama hicho kilinusurika kubomolewa

Wapangaji wa nyumba hiyo walihoji ni serikali gani inaruhusu jengo kuvujwa siku ya jumamosi septemba 29,,pamoja na kuhoji pia waliwalalamikia wanaoshiriki zoezi la kubomoa kuwa wamesababisha kuuibiwa kwa vitu vyao pamoja na fedha zilizokuwa ndani ya nyumba

Viongozi wa CUF wamelaani kuvunjwa kwa ofisi zao kwa kuwa hawakupewa notice ya kuondoka katika jengo hilo

Akizungumzia kwa uchungu Naibu Mkurugenzi na siasa,habari na uwenezi Bw.Abdala Kambaya alisema kuwa tukio hilo lilihusishwa na siasa ambapo wanamtuhumu mwenyekiti na serikali ya CCM

Tukio hilo limejitokea wakati katibu mkuu wa chama hicho CUF ,Mh.Maalim Seif Sharif pamoja na viongozi wengine wa kitaifa wa chama hicho wakiwa tayari wamewasili  jijini  Arusha kwaajili ya mkutano wa hadhara

Hata hivyo hadi Jamii Blog inaondoka katika ofisi za CUF zilizopo kata ya Kaloleni ulinzi wa askari pamoja na wafuasi wa chama hicho walikuwa makini kulinda ofisi ya chama hicho kisivamiwe

Taarifa za ndani zinasema kuwa zoezi la bomoabomoa litaendelea asubuhi huku Mh.Maalim Seif akitarajiwa kufika katika ofisi hizo kwaajili ya kuweka saini,,,Je atasaini kitabu cha wageni barabarani?

Published by Pamela Mollel on September 29, 2012

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

1 maoni:

Anonymous said...

Huyo Mwenyekiti wa CCM Mohamed Ali Mkindi hana jipya hiyo ni familia potofu kwani baba zao walijenga majumba kwa kuiba matofali ya msikiti. hivyo kutumika kwa jambo la kuvunja nyumba hiyo haishangazi,kwani kwanza nyumba hiyo ina kesi ya dhuluma ya matajiri wa mji huo ambao hufanya watakavyo. Watoto wa marehemu wamedhulumiwa nyumba hiyo kwa ushirikiano wa matajiri,mawakili,na mah....na map..... MUNGU ATAWALANI WOTE. KWANI FAMILIA YA MKINDI HAMJIPIMI MUNGU ANAVYOWAADHIBU?

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO