Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Mwili wa aliekuwa Katibu wa BAWACHA Kata ya Unga Ltd - Arusha wazikwa leo

Mwili wa Bi Bertha Matai (44) aliekuwa Katibu wa BAWACHA Kata ya Unga Ltd umezikwa leo kijijini kwake Lawate-Lukanyi, Jimbo la Hai Mkoani Kilimanjaro ambapo viongozi mbalimbali wa chama chake walihudhuria sherehe za mazishi.

Miongoni mwa waliohudhuria maziko hayo ni pamoja na aliekuwa mbunge wa Arusha Mjini ambae rufaa ya kupinga kuvuliwa ubunge wake inatarajiwa kusikilizwa baadae mwezi huu, Mh Godbless Lema, na Mbunge wa Viti Maalumu (CHADEMA) Mh Joyce Mukya.

Wengine walioshiriki ni madiwani wa CHADEMA kutoka Hai, Moshi, Siha na Arusha, pamoja na viongozi wengine wa chama.

Mwili wa marehemu uliagwa katika hospitali ya Mt Meru na pia Ofisi ya chama Kata ya Unga Ltd kwa sala na dua kisha kabla ya kusafirishwa kwenda Moshi kwa maziko.

Bi Matai alifariki siku ya Alhamis tarehe 30 Agosti, 2012 baada ya kusumbuliwa na maleria kwa muda wa wiki moja. Alifikwa na mauiti katika hospitali ya Mt Meru alikohamishiwa kutoa Selian kwa matibabu zaidi.

Marehemu ameacha mume na watoto wawili ambao, mmoja yuko kidato cha pili na mwingine cha tatu.

Blog hii inawapa pole wafiwa wote, Mungu awape ujasiri,kifo hiki kiwe ukumbusho wa sisi tuliobaki kuishi kwa kutenda memo yanayompendeza Mungu. Mungu aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi. Amina!

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO