Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Jeshi La Polisi Launda Tume Ya Kuchunguza Kifo Cha Daudi Mwangosi

JESHI la Polisi nchini limeunda tume itakayochunguza kifo cha Mwandishi wa Habari wa Kituo cha Channel TEN, Marehemu Daud Mwangosi kilichotokea mjini Iringa wakati Jeshi la Polisi likipambana na wafuasi wa Chadema waliokuwa katika ufunguzi wa tawi la chama hicho katika Kijiji cha Nyololo mjini Iringa.

Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Polisi Paul Chagonja uchunguzi huo utavishirikisha vyombo vya usalama kutoka Jeshi la Polisi pamoja na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) 'kuwa Jeshi la Polisi limeunda tume  itakayowahusisha Maofisa kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ pamoja Mkurugenzi wa Makosi ya Jinai Robert Manumba, Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Said Mwema ili kubaini ukweli kuhusu kiliochosababisha kifo cha mwandishi huyo basi tusubiri matokeo ya uchunguzi huo' alisema Chagonja.

Marehemu Mwangosi amefariki dunia jana wakati baada ya kulipukiwa na kitu kinachachodaiwa kuwa ni bomu wakati chama cha Demokrasia na Maendelo (Chadema) kikifungua tawi la chama  katika Kijiji cha Nyololo, Mufindi Iringa.

Mwili wa Daud Mwangosi baada ya kusambaratishwa na bomu. Aliyekaa jirani ni askari (OCS) ambaye alijeruhiwa katika tukio hilo

Polisi wa FFU wakipiga mabomu ya machozi kutawanya wafuasi wa Chadema waliokuwa katika ofisi za tawi la chama chao

Mkuu wa Operesheni Sangara wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Benson Kigaila, akiwa katika gari la chama hicho pamoja na mmoja wa majeruhi wa vurugu za polisi na wafuasi wa chama hicho

RPC katika maandalizi

Viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema wakipandishwa katika gari la Polis

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO