Rais Jakaya Kikwete leo (jana) alikuwa na mkutano wa dharura wa wakuu wa nchi kutoka Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama (TROIKA) ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC).
Rais Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa asasi hiyo, ameitisha mkutano huo kwa ajili ya kuzungumzia mgogoro wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa jana kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, mkutano huo wa siku moja ulifanyika jijini Dar es Salaam kuanzia jana, Septemba 4, 2012.
Nchi ambazo ni wajumbe wa asasi hiyo ni Msumbiji ambayo ni Mwenyekiti wa sasa wa SADC, Afrika Kusini iliyokuwa Mwenyekiti wa asasi hiyo kabla yaTanzania na Namibia ambayo ni Makamu Mwenyekiti wa asasi hiyo ya Troika.
Wakuu wa nchi hizo waliwasili nchini kuanzia juzi kwa ajili ya kuhudhuria mkutano huo.
Zifuatazo ni picha toka ofisi kuu, Ikulu za mkutano huo.
0 maoni:
Post a Comment