Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Je, Uwezo Wetu Wa Kufikiri Umepungua? - tafakuri ya Maggid Mjengwa

Ndugu zangu,

Yanayotokea nchini mwetu yanatutaka sio tu tufikiri, bali, tufikiri kwa bidii. Lakini swali ni hili; Je, uwezo wetu wa kufikiri umepungua?

Yumkini si kwa aliyekuwa na ujasiri wa kuipiga picha hiyo hapo juu. Alifikiri sana pia. Na si kwa aliyekaa chumba cha habari na kuumiza kichwa, kisha akaamua picha hiyo ipambe sura ya mbele ya gazeti la Mwananchi la juzi. Hapa Iringa gazeti hilo liligombaniwa kama njugu, na bila shaka sehemu nyingine za nchi.

Naam, siku hizi utasikia ikisemwa; " Tumefika pabaya!" Mwingine atasema; " Tunakokwenda ni kubaya!". Lakini, ni Watanzania wangapi wenye kuuliza maswali haya; " Tumefikaje hapa?" Na " Je, tunaendaje?" Maswali hayo yanamtaka mwanadamu afikiri kwa bidii.

Wakati mwingine nafikiri, kuwa Watanzania tumechoka kufikiri. Hata kwenye maswali magumu yenye kutuhusu tunataka wengine wafikiri kwa niaba yetu. Unaweza kukutana na Mtanzania mwenzako ukamwuliza; " E bwana ee, unafikiri nini juu ya jambo hili?". Jibu lake; " Kwani wewe unaonaje?"- Ni moja ya maswali yenye kuashiria anaykujibu swali lako amechoka kufikiri.
Na wakati mwingine tatizo si kutofautiana kifikra, bali kutofautiana namna au jinsi ya kufikiri. Swali moja, lakini unaweza kuona namna tunavyotofautiana katika kuchagua njia ya kulisogelea ( approach) swali husika.

Na kuna wenye kukimbilia kutafuta njia za mkato. Ndio, majawabu ya mkato. Na baadaye itakuwaje? Inshallah na BwanaYesu Asifiwe!
Maggid Mjengwa,
Iringa
0788 111 765
mjengwablog.com

Source: http://www.wavuti.com/#ixzz25aOF2pNg

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO