WAKATI Rais Jakaya Kikwete akisema hakuna rushwa kwenye kashfa ya ununuzi wa rada kutoka nchini Uingereza, wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wamemkalia kooni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe, wakimtaka awataje watuhumiwa na kashfa hiyo.
Wabunge hao walitoa kauli hiyo bungeni jana alipokuwa wakichangia hoja ya bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Ushirikiano wa Kimataifa na kwamba mbali na kutajwa kwa watuhumiwa hao pia serikali iwachukulie hatua na si kufurahia tu chenji yake ambayo imerejeshwa nchini hivi karibuni. Soma zaidi Tanzania Daima….
0 maoni:
Post a Comment