Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

LEMA: USHAIDI WANGU KWAMBA RAIS KIKWETE NDIE KINARA WA UDINI UMEKAMILIKA

F 1

Taarifa iliyowekwa kwenye mtandao wa Jamii Forums na memba wa mtandao huo ambaye aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Vijana  CHADEMA Mkoa wa Arusha, Exaud Mamuya inaeleza kuwa Lema amekamilisha ushahidi wake kuhusiana na agizo la Spika wa Bunge kumtaka awasilishe ushahidi wa kauli yake aliyoitoa Bungeni kuwa Kinara wa Udini nchini ni Jakaya Kikwete.

Bandiko hilo la Mamuya linasomeka hivi…

“Mh Lema amethibitisha ya kwamba ushahidi alioagizwa kuuwasilisha kwa spika wa bunge ya kwamba Rais Jakaya Kikwete ni kinara wa udini tayari ameshaukamilisha.

Aliyasema haya hapo jana nilipokuwa nikizungumza naye ya kwamba aliamriwa kuuwasilisha katika vikao vya bunge vya wiki hii lakini akashindwa kufanya hivyo kutokana na uhuni wa Jeshi la Polisi nchini na idara ya usalama wa Taifa pamoja na uhuni wa anayejitambulisha kama Mkuu wa Mkoa wa kumkamata kama jambazi na kumuweka rumande kwa muda wa siku nne.

Lakini alisema tayari ameshamuandikia barua spika wa bunge ya kumtaarifu kilichotokea Arusha na kwamba ushahidi wake umeshakamilika na yuko tayari kuuwasilisha katika vikao vya bunge vya wiki ijayo.

Akidokeza juu ya ushahidi huo alisema uko katika video na nyaraka mbalimbali za maandishi ambapo kama spika ataridhia uwasilishwe ndani ya bunge basi chama cha mapinduzi (CCM) pamoja na chama kimoja cha upinzani vitaenda kufa kabisa kutokana na ushiriki wake katika udini huo. Lakini akasema endapo spika wa bunge ataamua kufanya uhuni wa kutoupeleka bungeni kama alivyofanya katika ushahidi wake ya kwamba WAZIRI MKUU NI MUONGO basi atakiomba chama chake kikubali ushahidi huo uwekwe katika mitandao ya kijamii pamoja na youtube ila kila Mtanzania na wasiokuwa watanzania waweze kuona Rais anavyoligawa Taifa la Tanzania.

Alisema kutokana na usalama wa ushahidi huo ameamua kumuita Arusha katibu wa Chadema mkoa wa Dar es salaam bwana Henry Kilewo kwa ajili ya kuuchukua na kuupeleka Dar ambapo utapelekwa Dodoma. Na tayari bwana Kilewo ameshauchukua na kuupeleka Dar kwa ndege ya fast jet iliyoondoka jana usiku saa tatu. So Jumapili mh Lema atakapokuwa anaelekea Dodoma atakuwa hajabeba ushahidi huo bali ataukuta Dodoma.

Pia katika video hiyo yumo Shekh Ilunga wa Morogoro akifanya vikao na viongozi hao (Rais pamoja na kiongozi huyo mkuu wa chama cha upinzani)” mwisho wa kunukuu

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO