RUFAA ya kupinga kuvuliwa ubunge wa aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (CHADEMA), imesikilizwa leo na jopo la majaji watatu wa Mahakama ya Rufaa, wakiongozwa na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande, na kisha kuahirishwa hadi siku ambayo itatangazwa baadae
Viwanja vya Mahakama Kuu Arusha vikiwa vimefurika watu wakati wa mjadala wa rufaa ya Lema. Hapa kama picha inavyoonesha, rufaa imekwisha ahirishwa na wananchi hawa wanaondoka maeneo hayo..
Baadhi ya wananchi waliokusanyika nje ya ofisi za Chadema Mkoa wa Arusha, eneo la Ngarenaro wakimsikiliza Mh Godbless Lema haonekeni pichani mara baada ya kutoka Mahakamani kusikiliza shauri lake kupinga kuvuliwa ubunge. Picha hii ni taswira nusu ya kwanza ya watu
Mh Lema akizungumza kuagana na wananchi waliokuwa nae Mahakamani, mbele ya ofisi za chama hicho muda mfupi uliopita
Hii ni nusu nyingine ya taswira halizi za wananchi waliofika ofisini hapo
Shamrashamra barabarani wakitoka Mahakamani hii leo
Wafuasi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wakiandamana kutokea mahakamani,ambapo rufaa ya aliekua Mbunge wa Chadema jijini Arusha Bw. Godbless Lema, ilisikilizwa na kusogezwa mbele. Wafuasi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wakiandamana kutokea mahakamani,ambapo rufaa ya aliekua Mbunge wa Chadema jijini Arusha Bw. Godbless Lema, baada ya kusogezwa mbele. Wafuasi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)wakiongozana na aliekua Mbunge wa Chadema jijini Arusha Bw. Godbless Lema Mbunge kutokea mahakamani ambapo rufaa yake ilisikilizwa. Aliekua Mbunge wa Chadema jijini Arusha Bw. Godbless Lema akionekana juu ya gari pamoja naWafuasi wa Chama hicho wakitokea mahakamani. Wafuasi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wakibembea juu ya gari la Mbunge. Gari lilipopambwa kwa nakshi za M4C likifuata msafara wa Aliekua Mbunge wa Chadema jijini Arusha Bw. Godbless Lemawakitokea mahakamani. Picha nne za mwisho na Audiface Jackson Blog!
0 maoni:
Post a Comment