Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Mkutano Mkuu wa Watanzania waishio Ujerumani mwaka 2012 wafana mjini Frankfurt

Mkutano mkuu wa watanzania waishio ujerumani  uliofanyika siku ya jumaamosi tarehe 29. 09 2012 Mjini Frankfurt katika kitongoji cha Raunheim. ulifanikiwa kutimiza malengo yake na maazimio yake  moja wapo ilikuwa ni kufanya uchaguzi wa uongozi wa umoja huo.

Kabla ya kufanyika kwa uchaguzi huo na mjadala  wa maazimio ya umoja huo. Mgeni rasmi katika mkutano huo mwana diplomasia Naibu Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani, Mheshimiwa Bw. Ali Siwa alitoa nasaha zake na salamu kutoka Ubalozi wa Tanzania nchini Ujerumani kwa watanzania waliohudhuria katika mkutano huo. Kwanza aliwapongeza watanzania kwa kufanikiwa kuunda umoja huo wa watanzania waishio ujerumani ambao ndio mwamvuli mkuu wa mshikamano wa watanzania wote nchini Ujeruman.

Bw. Ali  Siwa aliwaambia watanzania kwamba ofisi yake ipo wazi wakati wowote iwapo umoja huo utahitaji ushauri wowote utakaoleta  maendeleo ya umoja huo na watanzania kwa ujumla, aliwaasa watanzania kuwa mshikamano wao na umoja wao ndio utakaokuwa ufunguo  na sauti ya maendeleo yao na vizazi vwao ugenini na nyumbani pia.

Baada ya nasaha hizo  wananchama wa umoja wa watanzania  walichagua viongozi wao kama ifuatavyo:-Mwenyekiti: Mfundo Peter Mfundo, Makamo: M/Mwenyekiti. George Mtalemwa. Katibu: Bi Tulalumba Mloge. Muweka hazina: Bi Mwamvua Dugala Merkel.Umoja huo wa Watanzania Ujerumani (UTU) ndio chombo pekee kilichopata usajili kwenye serikali ya ujerumani, na kutambuliwa kisheria,  ambacho kinawaunganisha watanzania wote wanaoishi ujerumani, na ndio Daraja linalowaunganisha  watanzania waliopo Nyumbani na kwengineko ughaibuni. Kwa watanzania wanaopenda kujiunga na umoja wa watanzania ujerumani (UTU) milango ipo wazi,  wasiliana na  kamati.utu@googlemail.com

Naibu Balozi Mh.Ali Siwa (mwenye suti nyeusi) akiwa na viongozi wa UTUNaibu Balozi Mh.Ali Siwa (mwenye suti nyeusi) akiwa na viongozi wa UTU

Kamanda Ras Makunja wa FFU (mwenye kofia) akiwa chini ya ulinziKamanda Ras Makunja wa FFU (mwenye kofia) akiwa chini ya ulinzi

Meza kuu katika mkutano wa Umoja wa watanzania UjerumaniMeza kuu katika mkutano wa Umoja wa watanzania Ujerumani

Watanzania Ujerumani wakiduarikaWatanzania Ujerumani wakiduarika

watanzania Ujerumani wakiwa na furaha ya umoja waowatanzania Ujerumani wakiwa na furaha ya umoja wao

huyu bint mdogo naye alikuapoHuyu bint mdogo naye alikuapo. Picha zote na Msemakweli wa Ngoma Afrika Band, Ujerumani

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO