Kilio cha wakulima wengi ni kupunjwa katika bei ya manunuzi ya bidhaa zao wanazozalisha wakilinganisha na gharama walizotumia hadi kupata mavuno.
Mara nyingi wafanyabiashara ndio wameonekana kunufaika na faida ya Kilimo ukilinganisha na mkulima husika. Mfanyabiashara huyu anajikuta anapata faida kubwa katika kipindi kifupi tofauti na mkulima ambae amehangaikia mazao yake shambani kwa muda mrefu.
Zipo jitahada mbali mbali zimefanyika katika kumuwezesha huyu mkulima nae angalau anufaike na jasho lake kwa kiwango fulani, ukiwemo utaratibu wa Serikali wa Stakabadhi kwa mazao ghalani. Utaratibu ambao nao unakailiwa na changamoto za urasimu na rushwa.
Pia uwepo wa middlemen ulikuwa ukiwapunja sana wakulima hapo awali. Kwasasa utaratibu huo haupo sana.
Wiki hii Blog yako ilitembelea masoko ya ndizi ya Mwika (Moshi Vijijini) na Masera (Rombo). Kila siku ya Ijumaa na Jumanne wananchi wengi, hasa kinamama wamekuwa wakipeleka ndizi wanzovuna shambani kwao ili kufanya biashara na wafanyabiashara wanaozisafirisha kwenda maeneo tofauti ya nchi na nje ya nchi.
Ndizi nyingi kutoka masoko haya zinaelezwa kuwa husafirishwa kwenda mikoa ya Tanga, Arusha na Dar es Salaam. Nyingine husafirishwa kwenda nchi jirani ya Kenya.
Si ndizi pekee, kuna matunda mengine kama parachichi (avocado) nayo husafirishwa kwa wingi. Gunia moja la parachihci kwa sasa limeshuka toka sh 45,000 wakati yakiwa hadimu hadi sh 30,000 kipindi hiki yako mengi.
Wakulima wa ndizi wanalalamikia bei ndogo kwa mazao yao hayo hasa kipindi hiki cha ‘mafuriko’ ya mavuno ambapo mkungu mmoja wa ukubwa wa wastani huuzwa kwa kiwango cha sh 6000 na 7000 mbapo mkungu huo huo ukifika Dar es Salaam huuzwa kwa zaidi ya 20,000.
Wenyeji wanasema mara nyingi wakati wa sikukuu bei huwa nzuri na kushuka kipindi cha kufungua shule mabapo wazazi wengi huuza mifugo yao na ndizi ili kupata fedha za kulipia ada watoto wao na hivyo kupelekea soko la ununuzi kuwa dogo kulinganisha na wauzaji.
Hapa kinamama wafanyabiashara wa Mwika (na maeneo mengine jirani) wakiangalia namna ya kuuza ndizi zao juzi
picha chini na juu: msururu wa malori ambayo yapo tayari kupakia ndizi sokoni hapo na kuzisafirisha kwa walaji. Serikali huchukua ushuru kwa kila gari
0 maoni:
Post a Comment