Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

News Alert: UCHAGUZI WA WABUNGE BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI: WASHINDI KUJULIKANA SAA MOJA JIONI

Zoezi la upigaji kura kuwapata wabunge tisa watakaoiwakilisha Tanzania katika Bunge la Jumuia ya nchi tano za Shirikisho la Afrika Mashariki limefanyika katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa tanzania Mjini Dodoma.

Uchaguzi huo umefuatia zoezi la kila mgombea kujieleza mbele ya wabunge na kuulizwa maswali, chini ya usimamizi wa Spika wa Bunge, Mh Anna Makinda.

Moja ya sifa za mtu kuruhusiwa kugombea nafasi hii muhimu ya uwakilishi ni kuwa Matanzania.

Sifa nyingine zinamtaka mgombea awe na sifa zinazomruhusu kugombea na kuchaguliwa kuwa Mbunge katika Bunge la Jamhuri ya Muungano, pia asiwe na wadhifa wa uwaziri katika Serikali ya nchi wananchama.

Halikadhalika mgombea  wa nafasi hii hakupaswa kuwa afisa mtendaji katika Jumuia, na awe ameonyesha utashi na shabaha ya kuendeleza Jumuia ya Afrika Mashariki.

Jumla ya wabunge 9 wanahitajika kupatikana jioni ya leo ili kuiwakilisha nchi katika Bunge la pamoja (EALA). Wabunge hao 9 watapatikana katika makundi manne ya uwakilishi.

Makundi hayo na kura zake kwenye mabano ni Wanawake (2), Wawakilishi toka Tanzania Zanzibar (2), Upinzani (2), na Wawakilishi toka Tanzania Bara (3).

Kila mpiga kura ametakiwa kuchagua wagombea katika kila kundi kwa idadi ambayo inahitajika kwa kila kundi.

Jumla ya wapigakura 302 (Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania) wakiongozwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Mh Freeman Mbowe ndio waliojitokeza kushiriki zoezi hilo.

Kwa kawaida Bunge la Afrika Mashariki huwa na wajumbe 45 wa kuchaguliwa na wengine 5 wanaoingia kwa nafasi zao. Mfano ni mawaziri toka nchi wanachama wanao shugulikia maswala yanayohusu Jumuia hiyo.

Aidha, katika kabla ya zoezi la kupiga kura kuanza, kuliibuka wasiwasi miongoni mwa wabunge pale Katibu wa Bunge alipotoa maelekezo na kueleza kuwa wabunge wawe makini kura zao zisiharibike na kwamba kila fomu ina ‘serial no.’ ambayo mhusika ambae kura yake itaharibika atajulikana.

Hofu hiyo iliibuliwa na Mh Blandesi alieomba muongozo wa Spika na kueleza kuwa kama utaratibu ndio huo ulioelezwa na Katibu basi zoezi la upigaji kura halitakuwa siri tena.

Hata hivyo, Spika makinda aliingilia kati na kuwatoa hofu waheshimiwa wabunge kuwa namna hiyo ya siri ni haihusiki kuwatambua wapiga kura.

Hoja nyingine iliyoibuka kabala ya upigaji kura kuanza ilihusu nafasi mbili za wawakilishi toka Zanzibar ambazo hazikufafanuliwa kama ni moja kwa wanawake au wanaume.

Hoja hii ilijibiwa na Spika kuwa nafasi mbili kwa Zanzibar ni kwa watu wa jinsia zote kutegemeana na mpigakura atakavyoamua na kwamna nafasi kwa wanawake zipo katika kundi maalumu la wanawake.

Hata hivyo, vyama vya upinzani vilipoteza nafasi ya kuweza kuchaguliwa kuwakilisha Zanzibar na kuachia nafasi hiyo CCM pekee ambayo ilipeleka wagombea 9. Haikuweza kufahamika kama ni hawakufahamu hilo hapo kabla au labda maelekezo ya awali hayakueleweka.

Katika tukio jingine, mbunge mmoja  toka Zanzibar aliomba muongozo wa Spika na aliporuhusiwa alitaka kujua kama anaruhusiwa kuigilizia kura yake kwenye kijikaratasi ambacho amekiandaa kikiwa na majina ya watu anaowataka kuwapigia kura. Spika Makinda aliruhusu kuigilizia kwa sababu kikaratasi hicho hakitahesabiwa katika kuhesabu kura, bali ni fomu maalumu za kupigia kura.

Kikao kitaahirishwa baada ya zoezi la kupiga kura kukamilika na wabunge watarudi tena majira ya jioni saa moja ili kupata matokeo

Chanzo: Matangazo ya moja kwa moja toka Bungeni kupitia Star Tv na TBC

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO