Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua utengenezaji vyandarua na nguo katika kiwanda cha A to Z cha Arusha Aprili 15,2012. Kushoto ni Mtendaji Mkuu wa kwanda hicho, Anuj Shah. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu, kwa hisani ya Daily Mitikas Blog)
Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh Mizengo Kayanza Peter Pinda, leo alifanya ziara katika kiwanda cha nguo cha Sun Flag kilichoko eneo la viwanda Themi, Jijini Arusha.
Katika hotuba yake, mara baada ya matembezi kuangalia jinsi uzalishaji wa nguo na vitambaa unavyofanyika kiwandani hapo Waziri Mkuu alisema Serikali itaviwezesha viwanda vya nguo vya ndani ili viweze kuzalisha kwa ufanisi zaidi.
Sunflag (Tanzania) Limited ilianzishwa mwaka 1965 na kwa sasa imeajiri zaidi ya watu 2700 kutoka nyanja zote za maisha.
Jiwe la msingi la kiwanda hiki liliwekwa mapema miaka ya 1930 na Mwenyekiti wa Sunflag Group, Bw. Satya Dev Bhardwaj, wakati alipoanzisha kiwanda cha kwanza nchini Kenya.
Hadi kufikia leo, Sunflag Group wanafanya kazi za uzalishaji nguo sehemu mbalimbali duniani kupitia ofisi na viwanda vyao vilivyoko United Kingdom, India, Thailand, Kenya, Nigeria, USA na hapa nyumbani Tanzania.
maelezo ya ziada yamepatikana kwenye website ya kiwanda
0 maoni:
Post a Comment